Arsenal hapo jana imepeleka
wameonyesha kuwa wanaweza kuwa mwiba mkali katika ligi kuu ya England
kwa msimu huu baada ya kuibamiza bila timu ngumu ya Manchester City kwa
jumla ya mabao 3- kwa nunge katika mechi ya ngao ya Jamii mechi
iliyopigwa kwenye uwanja wa Wembly.
Mabingwa hao wa kombe la FA walianza kwa
kupeleka kilio kwenye kambi ya Man City kwa goli la kwanza lililofungwa
na Santi Cazorla dakika 21 kipindi cha kwanza.Kama hiyo haitoshi Aaron Ramsey dakika ya 42 aliweka mpira wavuni kuandika goli la pili na kuwafanya Man city wazidi kupata kizungungu na kutojua la kufanya kabla ya Oliver Giroud kumalizia karamu ya Arsenal kwa kushindilia msumari moto kwenye kidonda kwenye dakika ya 60 kipindi cha pili na hivyo kusambaratisha vijana hao wa Manuel Pellegrini kwa jumla ya magoli 3 - 0.
No comments:
Post a Comment