TANGAZO


Monday, August 11, 2014

Mapigano yasitishwa tena Ukanda wa Gaza





Harakati za amani kutaka vita vikomeshwe Gaza

Israel na Palestina wamekubaliana kusitisha mapigano tena Gaza kwa saa 72 - makubaliano yaanza kutekelezwa Jumapili saa 6 za usiku kwa saa za Afrika Mashariki
Wapatanishi wa Misri wamesaidia kuwezesha makubaliano hayo kufikiwa na mapigano yakisita kweli, Jumatatu Israel itatuma wawakilishi mjini Cairo kwa mazungumzo ya kutafuta suluhu ya muda mrefu katika mzozo huo.
Mwandishi wa BBC mjini Jerusalem anasema Israel itaendelea kudai kuwa Gaza liwe eneo lisilokuwa na silaha - na Hamas itataka Israel iache kuizingira Gaza na iondoe vizuizi vya kuingia na kutoka.
Watu zaidi ya 20 wameuwawa tangu usitishwaji wa mapigano wa mwisho kumalizika Ijumaa.

No comments:

Post a Comment