TANGAZO


Monday, August 11, 2014

Marekani kuendelea kuishambulia Iraq





Wapiganaji wa Kurdi

Marekani imeendeleza mashambulizi ya anga kaskazini mwa Iraq kwa lengo la kuwasaidia Wakrud katika mji wa Erbil dhidi ya wapiganaji wa kiislam wa kundi la Jihad.
Wapiganaji wa kundi hilo la Kiislam hivi karibuni wameendelea kuimarisha ngome yao katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuiteka ngome kubwa ya Iraq katika mji wa Mosul.
Jeshi la Marekani limesema limefanya mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Sunni waliokuwa wamejificha katika milima iliyo eneo la wakimbizi la Yazid.
Hata hivyo Uingereza imesema inaendelea kutoa misaada ya kibinadamu kwa Wakurdi ambapo Ofisa wa zamani wa mambo ya kigeni wa Uingereza Alistair Burt anasema nchi hiyo inaweza kusaidia eshi la Wakurdi.
Wakati huo huo vikosi vya majeshi ya Iraq na vyombo vya usalama vimesambaa katika katika maeneo mbalimbali ya mji wa Baghdad huku kukiwa na hali ya wasiwasi kufuatia kauli iliyotolewa na waziri mkuu wa nchi hiyo ya Iraq Nouri al-Maliki inayodaiwa kuwa ni ya utovu wa nidhamu kwa Rais wa nchi hiyo Fuad Masum.
Amesema kuwa Rais wa Jamhuri hiyo amevunja katiba mara mbili,mara ya kwanza ni pale alipojiongezea muda wa kukaa madarakani,wakati alistahili kutangaza kuvunja bunge. Hata hivyo kipindi chake kiliisha august saba alhamisi iliyopopita.
Hata hivyo papa Francis ameelezea gogoro wa Ira kwamba msingi wake mkubwa ni masuala ya tofauti za kidini. Melfu ya watu nchini Iraq wamekuwa wakilazimishwa na wapiganaji wa kiislam ambao wameimarisha ngome ao kaskazini mwa nchi hiyo.Katika ujumbe wake wa jumapili ,papa Francis ametoa wito kwa dunia kukomesha uhalifu huo unaoendelea nchini Iraq.

No comments:

Post a Comment