Serikali ya Misri imewanyima vibali vya kuingia nchini humo maafisa wawili wa kupigania haki za kibinadamu ikihofia usalama wao.
Mkurugenzi mkuu Kenneth Roth na bi Sarah Leah
Whitson walikuwa mjini Cairo kuzindua ripoti maalum kuhusiana na mauaji
yaliyotokea wakati wa maandamano yaliyopelekea kupinduliwa kwa serikali
ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mojhammed Morsi.Mamia ya watu waliripotiwa kufariki mnamo tarehe 14 Agost1 2013 baada ya maafisa wa Usalama kutibua maandamano ya kupinga kung'olewa madarakani kwa Morsi.
Rais Abdul Fattah al-Sisi, alikuwa mkuu wa majeshi wakati huo yalipotokea mauaji hayo.
Shirika hilo la Human Rights Watch (HRW) lilikuwa mstari wa mbele kushtumu mauaji ya wapinzani wa serikali kufuatia kung'olewa madarakani kwa Morsi mwezi Julai mwaka uliopita.
Bi Whitson,ambaye ni afisa mkuu wa HRW katika eneo la Mashariki ya Kati alisema kuwa walielezwa kuwa walikuwa wakifurushwa nje ya Misri kwa sababu za kiusalama.
Kulingana na HRW hii ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa maafisa wao kunyimwa ruhusa ya kuingia ndani ya Misri hata wakati wa utawala wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hosni Mubarak.
Katika ripoti hiyo itakayozinduliwa hapo kesho "maafisa wa polisi na jeshi la Misri walifyatulia waandamanaji risasi " haswa baada ya kung'olewa madarakani kwa aliyekuwa rais Morsi.
Zaidi ya watu 1,150 waliuawa katika maandamano 6 kati ya mwezi Julai na Agosti mwaka uliyopita.
Maafa zaidi yaliripotiwa katika medani ya Nahda na karibu na Msikiti wa Rabaa al-Adawiya ulioko Cairo.
Roth alisema kuwa Human Rights Watch ilikuwa imekwisha iarifu utawala wa Misri kuhusu ripoti hiyo na ilikuwa inatarajia kujadiliana na serikali ya rais Sisi.
Serikali haijapinga wala kukubali madai hayo.
No comments:
Post a Comment