Mwenyekiti
wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta ameunda kamati ndogo yenye ujumbe
wa watu 10 kwa ajili ya kushughulikia masuala ambayo hayakufikia muafaka wakati wa majadiliano ya
kupitia sura mbalimbali za Rasimu ya Katiba Mpya kwenye Kamati 12 za Bunge hilo.
Kamati hiyo
itakuwa inaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe. Samia Suluhu
Hassan,ambapo wajumbe wa kamati hiyo wametoka kila pande ya
Muungano yaani watano wametoka Tanzania
Bara na watano kutoka Zanzibar.
Aidha Mhe.
Sitta akizungumzia kuhusu maendeleo ya kazi za Kamati hizo, ambapo alisema zinaendele vizuri, hivyo
kuanzia wiki ijayo sura zote 15 zitakuwa zimepigiwa kura,hivyo Kamati hizo zitakuwa zimemaliza sura 17 ya rasimu
hiyo na za nyongeza ifikapo Agosti 27,mwaka huu ili kuanza kuwasilisha katika Bunge hilo
kuanzia Septemba 2,mwaka huu.
Hayo yalisemwa leo na Mhe.
Samuel Sitta wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokutana nao leo
kuhusu muhtasari wa kikao cha Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo kilichokaa leo
kutathmini kazi za Kamati 12 za Bunge hilo lilipofikia pamoja kuridhia baadhi
ya mapendekezo ya kuongeza Ibara na sura ndani Rasimu ya Katiba katika Kamati
zao.
Mwenyekiti
huyo aliyataja mambo ambayo yatashughulikiwa na kamati hiyo, ni muundo wa Bunge
katika masuala ya Muungano, uraia
pacha, mahakama ya kadhi na kamati ya pamoja ya fedha.
“Haya mambo
manne nimeagiza ufanyike utaratibu maalum,” alisema Mhe. Sitta.
Mhe . Sitta akizungumzia kuhusu tathimini ya mwenendo wa
Kamati hizo, alisema zipendekeza masuala kadhaa na kuacha mengine kama yalivyo katika rasimu hiyo.
Akizungumzia
kuhusu yaliyojadiliwa katika kikao cha Kamati ya Uongozi ya Bunge hilo,kabla ya
kukutana na waandishi wa habari, Mhe. Sitta alisema kamati hiyo imepokea
mapendekezo kutoka katika kamati mbalimbali kuhusu kuongezeka kwa sura na Ibara
za rasimu hiyo.
Aliyataja mapendekezo
hayo , likiwemo la Tume ya Marekebisho
ya Katiba lililowasilisha na Jaji Warioba kuhusu ardhi, mazingira na rasilimali
za taifa, Jumuia ya Tawala za Serikali za Mitaa (ALAT) na pendekezo la Haki
ya Watumiaji huduma na bidhaa ili kuwalinda walaji lililowasilishwa , Hawa
Ng’umbi ambaye ni mjumbe wa Bunge hilo.
Aliyataja mapendekezo mengine
ni la Jukumu la Serikali kujenga
uchumi imara, ambapo lengo ni kuwa na maendeleo ya uchumi wa ujamaa na
kujitegemea na Kuwepo kwa Baraza la Habari, la wajumbe wa 201 kuhusu ardhi,
wafugaji, wavuvi pia na wachimbaji wadogo ili ziweze kutungwa Sheria za
kusimamia masuala hayo.
Mhe. Sitta alisema kutokana na mapendekezo hayo kutakuwepo na ongezeko la ukurasa na
sura kadhaa katika rasimu hiyo.
Alisema Kamati
imebaini tatizo la mahudhurio, aliwapongeza
wajumbe wa Bunge hilo kutoka upande wa Zanzibar kwa kuwa na mahudhurio mazuri
kwenye vikao kuliko kutoka Tanzania Bara
kuacha visingizio vya kutohudhuria vikao.
Katika hatua
nyingine Mhe. Sitta alisema kutakuwepo na wataalamu kabla ua kumalizika kwa wiki hii kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa
mambo kadhaa kutoka Hazina kwa pande zote
za Muungano, ambapo ataukuwepo pia Gavana wa Benki Kuu, Profesa Bonaventure
Rutinwa kwa ajili ya suala la uraia pacha, uhamiaji na Profesa Issa Shivji ambaye ataoa ufafanuzi
juu ya aina ya Muungano ili kuwa na uwiano kwa kuwa hivi sasa yapo mambo machache.
No comments:
Post a Comment