Meneja
Habari, Elimu na Mawasiliano toka Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi Sylvia Lupembe
akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu jitihada wanazofanya
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kukabiliana na changamoto katika sekta
ya elimu,wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu
wa kitengo cha Masoko na Uhusiano toka benki ya KCB Bi. Christina Manyenye.
Baadhi
ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakiwasikiliza wawasilishaji
toka Mamlaka ya Elimu Tanzania, KCB, TOTAL, Social Action Trust Fund (SATF) leo
Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Hassan Silayo-MAELEZO)
Mkuu
wa kitengo cha Masoko na Uhusiano toka benki ya KCB Bi. Christina Manyenye
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mipango waliyoiweka kwa
kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania katika kuendeleza na kuinua sekta ya Nchini.kushoto
ni Meneja Sheria na Uhusiano toka kampuni ya uuzaji na usambazaji wa mafuta ya
TOTAL Bi. Masha Msuya.
Ofisa
Rasilimali Fedha toka taasisi isiyo ya kiserikali ya Social Action Trust Fund
(SATF) Bw. Timotheo Tenga akiwaeleza jambo waandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Sheria
na Uhusiano toka kampuni ya uuzaji na usambazaji wa mafuta ya TOTAL Bi. Masha
Msuya.
Frank
Mvungi-Maelezo
Mamlaka ya Elimu Tanzania inatarajia kukabidhi madawati
2000 kwa shule za Msingi 10 zilizopo jijini Dara es Salaam katika kukabiliana na Tatizo
la upungufu wa madawati hapa nchini.
Hayo yemesemwa na Meneja Habari Elimuna Mawasilano wa Mamlaka ya hiyo,
Bi Sylvia Lupembe wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam.
“Wanafunzi zaidi ya 6000
watanufaika na madawati hayo ambayo yatagharimu zaidi ya shilingi milioni mia moja na hamsini
(150,000)” alisema Lupembe.
Akifafanua zaidi Bi. Lupembe amesema shule zitakazo nufaika pamoja na Chamazi, Mbande, Boko
NHC, King’ong’o, Hekima, Bwawani, Bunju, Goba, Kombo na Kingugi.
Katika kuhamasisha wadau wengine kushiriki kwenye mchakato wa kuchangia madawati
Bi. Lupembe amesema kuwa Mamlaka ya ElimuTanzania (TEA), imezingatia rai iliyotolewa na Waziri Mkuu ikielekeza kuwa tatizo
la madawati katika shule za msingi limalizike ifikapo mwezi Juni, 2015 kwa kulipa kipaumbele suala hilo.
Pia
Bi. Lupembe alibainisha kuwa tathmini ya mwaka
2013 Tanzania ina upungufu wa madawati 1,147,471 hivyo, ni jukumu la
kila mdau kuunga mkono juhudi hizo ili kuondoa tatizo hilo kote nchini.
Naye Mkuu wa Kitengo cha
Masoko na Mahusiano wa benki ya KCB, Bi. Christina
Manyenye amesema wamekuwa wakishiriki katika kuchangia madawati ambapo kwa mwaka jana walichangia zaidi ya madawati 700.
“Tutaendelea kusaidia huduma za jamii katika maeneo mablimbali kama tunavyofanya katika sekta ya Elimu”, alisisitiza Manyenye.
Mamlaka ya Elimu Tanzania
(TEA), kwa kushirikiana na Kampuni ya Mafuta ya TOTAL na wadau wengine kama Kenya Commercial
Bank (KCB) na Social Action Fund wamekuwa katika ushirikiano tangu mwaka 2013
katika kutatua changamoto mbalimbali zinazo ikabili sekta ya Elimu hapa nchini, ikiwemo ya upungufu wa madawati.
No comments:
Post a Comment