Ethiopia na Kenya zimetangaza
niya ya kutaka kuwa wenyeji wa kombe la mataifa bingwa barani Afrika
mwaka wa 2017 baada ya Libya kujiondoa.
Libya ilitangaza kauli hiyo baada ya mapigano
kuchacha baina ya makundi mawili hasimu yaliyowanyima waandalizi fursa
ya kujenga viwanja vipya vya mashindano hayo.Ethiopia, ambayo imewahi kuwa mwenyeji wa mashindano hayo katika miaka ya 1962, 1968 na 1976, imesema kuwa itawasilisha rasmi ombi lake mara moja
"Serikali inaari ya kuyaleta mashindano hayo hapa Ethiopia ."alisema
Kenya kwa upande wake imetangaza niya ya kuandaa mashindano hayo kwa pamoja na Tanzania Uganda au Rwanda.
Shirikisho la soka barani Afrika limetangaza tarehe 30 Septemba kuwa siku ya mwisho ya mataifa kuwasilisha maombi yao.
Tangazo rasmi ya nani atakayeandaa mashindano hayo itakuwa mwakani .
No comments:
Post a Comment