TANGAZO


Tuesday, August 26, 2014

Obama apitisha ndege za uchunguzi: Syria





Rais Barack Obama

Rais wa Marekani Barack Obama ameidhinisha ndege za ufuatiliaji juu ya Syria ili kupata habari zaidi kuhusu shughuli za taifa la kiislamu (IS).
Wanahabari wanasema huenda uamuzi huo unadokeza mwanzo wa mashambulizi ya angani na Marekani ndani mwa Syria, ambako wanamgambo wa jihad wanathibiti maeneo kadhaa.
Tayari Marekani inatekeleza mashambulizi dhidi ya wanamgambo hao katika nchi jirani ya Iraq. Jumatatu, serikali ya Syria ilisema itashirikiana na jumuiya ya kimataifa dhidi ya IS.

Kufikia sasa serikali za magharibi zimepuuza mapendekezo ya kushirikiana na rais Bashar al-Assad katika jaribio la kukabiliana na tishio la IS katika maeneo kadhaa.
Wametoa wito kwa bwana Assad kujiuzulu tangu mwanzo wa upinzani mkali dhidi ya utawala wake kwa miaka mitatu na nusu sasa, ambapo zaidi ya watu 191,000 wanaaminiwa kuuwawa.

Maafisa wa Marekani walisema Rais Obama aliidhinisha ndege za upelelezi na pia huenda ndege za kijasusi za zikatumika.
Wanajeshi wa Marekani wamekuwa wakifuatilia IS kutoka angani nchini Iraq kwa miezi kadhaa na kutekeleza mashambulizi ya anga ya 8 Agust mwaka huu dhidi ya IS iliyokuwa kiungo cha Al-Qaeda.

Rais Obama amekuwa akipinga kwa muda mrefu kutekelezwa kwa operesheni ya kijeshi nchini Syria, lakini inasemekana kuwa maafisa wa Pentagon walimshauri kuwa kufuata IS walipo na kukabiliana nao ndiyo njia pekee ya kukomesha tishio lao.

No comments:

Post a Comment