Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka.
Kamishna wa Kazi wa Wizara ya Kazi na Ajira, Saul Kinemela (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akikanusha taarifa zilizotolewa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), zilizodai Serikali inampango wa kupunguza mafao ya Pensheni ya wanachama wa Mifuko ya LAPF na PSPF. Kulia ni Kamishna wa Kazi Msaidizi, David Kanali na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Juma Muhimbi.
Kamishna wa Kazi Msaidizi, David Kanali (kulia), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari.
Meneja Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika, akimkaribisha Kamishna wa Kazi wa Wizara ya Kazi na Ajira, Saul Kinemela, kuzungumza na waandishi wa habari.
Kamishna wa Kazi wa Wizara ya Kazi na Ajira, Saul Kinemela (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati akikanusha taarifa zilizotolewa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), zilizodai Serikali ina mpango wa kupunguza mafao ya Pensheni ya wanachama wa Mifuko ya LAPF na PSPF.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya SSRA wakiwa kwenye mkutano huo.
Wakurugenzi wa SSRA wakiptia taarifa hiyo, iliyotolewa na Wizara ya Kazi na Ajira, ikikanusha tamko la pamoja lililotolewa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), kuhusu madai yao ya upunguzwaji wa mafao ya mifuko ya Pensheni ya wanachama wa LAPF na PSPF.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara mbalimbali za SSRA, wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Matekelezo na Uandikishaji, Lightness Mauki, Mkurugenzi wa Tehama, Carina Wangwe, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani, Peter Mbelwa na Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na Rasilimali watu, Mohamed Nyasama.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka, akizungumza kwenye mkutano huo. Katikati ni Mkurugenzi wa Sheria wa SSRA, Ngabo Ibrahim, akiandika taarifa hiyo na kushoto ni na Meneja Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde.
Baadhi ya waandishi wa habari, waliokuwepo kwenye mkutano huo, wakiandika na kunukuu masuala mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa kwenye mkutano huo.
TAARIFA KAMILI YA WIZARA YA KAZI NA AJIRA KUHUSIANA NA SUALA HILO
Kufuatia tamko la pamoja la
Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya
Juu Tanzania (THTU), kupitia Vyombo mbalimbali vya Habari mnamo tarehe 22 na 23,
Julai2014 wakidai kwamba Serikali ina mpango wa kupunguza mafao ya Pensheni ya
Wanachama wa Mifuko ya LAPF na PSPF; Wizara ya Kazina Ajira ambayo ndiyo yenye dhamana
ya sekta ya hifadhi ya jamii Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo;
i. Wizara ya kazi na Ajira inachukua nafasi hii kukanusha vikali taarifa zilizotolewa na
CWT and THTU, ambazo kwa namna moja au nyingine zinalenga katika kuupotosha Umma.
Tunaomba Wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Umma kwa ujumla,
uelewe wazi kuwa si SSRA wala Serikali zimetoa tamko lolote kuhusiana na upunguzaji wa
Mafao ya pensheni kwa wanachama wa Mifuko ya PSPF na LAPF.
Kinachoendelea ni majadiliano na Wadau wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii yenye lengo la
kuboresha mafao ya wastaafu. Hata hivyo, pamoja na majadiliano hayo, hakuna maamuzi wala tamko lolote lililotolewa kuhusiana na upunguzwaji
wa Mafao ya Wanachama.
ii.
CWT na THTU, wakiwa ni moja kati ya Wadau wa
Sekta ya Hifadhi ya Jamii, wanayo haki kikatiba ya kukutana na kujadiliana masuala mbalimbali yakiwamo
ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii. Si vema wakafanya upotoshaji kuhusu jambo hili muhimu.
iii.
Serikali inapenda kuchukua fursa hii kuwatoa hofu Wastaafu na Wanachama wote
wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, hususan wale wa PSPF na LAPF
na Walimu wote kwa ujumla kuwa maamuzi yoyote kuhusiana na mafao yao yanafanyika kwa uwazi na kuwahusisha wadau wote.
iv.
Hivyo tunaomba wadau wote wa Sekta ya Hifadhi ya
Jamii kuwa watulivu na kujiepusha na maneno yoyote ya upotoshaji, ambayo mwisho wake
yanaweza kuwachanganya Wanachama, na hivyo kusababisha kupunguza ufanisi katika utendaji
wa kazi.
Imetolewana;
KATIBU MKUU
WIZARA YA KAZI NA AJIRA
No comments:
Post a Comment