TANGAZO


Friday, July 25, 2014

Amiri Jeshi Mkuu, Rais Kikwete ahudhuria Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa Julai 25, 2014

Kikosi cha Bendi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kikipita kwa Gwaride wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye viwaja vya Mashujaa, Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo. Rais Jakaya Kikwete ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo. (Picha zote na Idara ya Habari, Maelezo)
Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kikipita kwa Gwaride wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye viwaja vya Mashujaa, Mnazi Mmoja, Dar es Salaam leo. Rais Jakaya Kikwete ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (wapili kushoto), akimpokea Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye (wapili kulia), wakati alipohuduria katika maadhimisho hayo.
Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman, akipokelewa wakati alipohudhuria katika maadhimisho hayo jijini leo. Wapili kulia ni Mkuu wa Majeshi Jeneral Davies Mwamunyange.
Mkuu wa Majeshi Jeneral Mwamunyange, akimpokea Makamu wa Rais, Mohamed Gharib Bilal, alipowasili katika viwanja hivyo katika maadhimisho hayo.
Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein akisalimiana na baadhi ya viongozi waliokuwa kwenye maadhimisho hayo, wakati alipowasili viwanjani hapo.
Mgeni rasmi, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na baadhi ya viongozi, alipowasili kwenye viwanja hivyo, wakati wa maadhimisho hayo.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete, akisindikizwa na Mkuu wa Majeshi, Jeneral Davies Mwamunyange, kuelekea sehemu yake, alipowasili kwenye viwanja hivyo, wakati wa maadhimisho hayo.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete, akipokea heshima kutoka kwa Jeshi la Wananchi, mara baada ya kuwasili na kuanza rasimi shughuli za maadhimisho ya Siku ya Mashujaa viwanja hapo.
 Wanajeshi wakitoa heshima zao kwa Mashujaa walipoteza maisha yao kwa kuitetea nchi yao ya Tanzania.
Mmoja wa Kiongozi wa Dini ya Kiislamu, akisoma salamu kwenye maadhimisho ya siku hiyo ya Mashujaa.
Mmoja wa Kiongozi wa madhehebu ya Dini ya Kikristo, akisoma salamu kwenye maadhimisho ya siku hiyo ya Mashujaa.
Mmoja wa Kiongozi wa madhehebu ya Dini ya Kikristo, akisoma salamu kwenye maadhimisho ya siku hiyo ya Mashujaa.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete, akikabidhiwa Mkuki na Ngao kwa ajili ya kwenda kuuweka kwenye Mnara wa Mashujaa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa viwanja hapo. 
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete, akiweka Mkuki kwenye Mnara wa Mashujaa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa viwanja hapo.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete, akiweka Ngao kwenye Mnara wa Mashujaa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa viwanja hapo.

Mkuu wa Mabalozi wa Nje nchini, Balozi Juma Mpango wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, akiweka shada la maua kwenye Mnara wa Mashujaa.

No comments:

Post a Comment