TANGAZO


Friday, July 25, 2014

Rais Kikwete amuapisha Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete akimuapisha Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Shaban Ally Lila leo, jijini Dar es Salaam.


Jaji Kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jaji Shaban Ally Lila (kulia) akitiasaini hati ya Kiapo mbele ya Rais Jakaya Kikwete wakati wa hafla ya kuapishwa kwake leo, jijini Dar es Salaam. Katikati, mwenye miwani ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akishuhudia tukio hilo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini hati ya Kiapo cha Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Shaban Ally Lila, wakati wa hafla ya kuapishwa kwa jaji huyo leo, jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkabidhi hati ya Kiapo Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania, Mhe. Shaban Ally Lila, wakati wa hafla ya kuapishwa kwa jaji huyo leo, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kushoto), akimpongeza Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila, mara baada ya kuapishwa rasmi kushika wadhifa huo, katika hafla iliyofanyika Ikulu leo, jijini Dar es Salaam.


Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania, Mhe. Shaban Ally Lila, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahaka Kuu ya Tanzania mara baada ya kuapishwa rasmi kushika wadhifa huo, katika hafla iliyofanyika Ikulu leo, jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni JajiMkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman. (Picha zote na Frank Shija- MAELEZO)

No comments:

Post a Comment