Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (katikati), akizungumza jambo na Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Abdul Mpakate (watatu kulia) wakati wa kufuturu futari maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya Watoto Yatima na Waishio katika Mazingira Hatarishi wa Kituo cha Nawoda mjini Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe aliandaa futari hiyo kwa watoto zaidi ya 80 wanaolelewa katika kituo hicho.
Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Abdul Mpakate akitoa dua la kumshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), kwa kuandaa futari maalum kwa ajili ya Watoto Yatima na Waishio katika Mazingira Hatarishi wa Kituo cha Nawoda mjini Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe aliandaa futari hiyo kwa watoto zaidi ya 80 wanaolelewa katika kituo hicho.
No comments:
Post a Comment