TANGAZO


Saturday, July 19, 2014

Rais Kikwete aifungua rasmi Barabara ya Peramiho-Mbinga ya Kilomita 78

Sehemu ya Barabara ya Peramiho -Mbinga, yenye urefu wa Kilometa 78 iliyofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakivuta utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Peramiho-Mbinga yenye urefu wa Kilometa 78.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Peramiho-Mbinga 78Km huku akiwa  na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Mamia ya wakazi wa Mbinga wakifurahia wakati Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa anamshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa Utendaji wake mzuri wa kuwajali wakazi hao kwa kuwajengea miundombinu bora.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa kwanza kulia), akizungumza na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kabla ya uzinduzi wa barabara ya Peramiho-Mbinga 78km. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati), akimshukuru Balozi wa China nchini (aliye kushoto kwake), kwa kazi nzuri iliyofanywa na Mkandarasi kutoka China Kampuni ya Synohdro. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia pamoja na Mawaziri wengine waliohudhuria ufunguzi wa barabara hiyo.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na baadhi ya Makatibu Wakuu na Mawaziri waliohudhuria katika ufunguzi wa barabara ya Perahimo-Mbinga (Km 78)

No comments:

Post a Comment