KAMPUNI ya Tigo Tanzania jana, ilifuturisha
zaidi ya watoto yatima 40 kutoka jiji la Dar es Salaam kama ishara ya upendo na
kujali wakati wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Akizungumza katika
shughuli hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo ya simu
Makumbusho, Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu kutoka Tigo Bi. Doris Luvanda
alisema kwamba wanayofuraha kubwa sana ya kusherehekea kipindi hiki cha mwezi
mtukufu na watoto wenye hitaji kutoka kituo cha watoto Al-Madrasat Nurilud ya
Temeke Mikoroshini.
“Ramadhani ni wakati wa
kipekee ambapo waislamu duniani kote wanaachana na ratiba zao za kawaida na
kujikita katika shughuli za kijamii, kutoa misaada, kufunga na swala. Sisi kama
Tigo tunayofuraha kubwa sana ya kushirikiana na wateja pamoja na jamii
inayotuzungukakatika wakati kama hizi. Tunaamini ya kwamba ishara ndogo ya
upendo kama hii inaweza ikamgusa na kubadilisha maisha ya mtu kwa njia ya
kipekee kabisa,” alisema Luvanda.
Sheikh
Masoud Seni ambaye ni mlezi wa kituo cha Al-Madrasat
Nurilud aliishukuru Tigo kwa kitendo chao cha kuwaandalia futari watoto hao
huku akiwasihi kampuni hiyo kuendelea na moyo huo huo.
“Kwa
wale watakaotumia utajiri wao, usiku na mchana, kwa usiri na mbele ya umma, dhawabu
zao zipo kwa Mwenyezi Mungu. Kwao hakutakuwa na la kuogopa, wala cha kusononeka
(Kuran 2:274). Hakuna namna ingine ambayo utaweza kuwa mwenye haki bila yakutoa
kile ambacho unakipenda zaidi. Na chochote unachokitoa, Allah anakifahamu
vizuri (Kuran 3:92),” alitafsiri Sheikh Masoud kutoka kwenye kitabu kitakatifu
cha Kuran.
No comments:
Post a Comment