Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma
Kikwete wakiangalia mandhari ya mji wa Pangani wakati wa ziara ya kikazi
wilayani humo. Sehemu kubwa ya mji huo imo katika hatari ya kumezwa na bahari
kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na serikali imeahidi kujenga ukuta
pembezoni mwa mto Pangani ili kuzuia athari za kimazingira kutokana na
kuongezeka kwa kina cha maji.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipitia moja ya
hotuba zake akiwa ndani ya kivuko kipya cha MV Pangani II wakati akivuka mto
Pangani kutoka Tarafa ya Bweni kuelekea Pangani mjini wakati wa ziara yake ya
kikazi wilayani Pangani jana. Rais Kikwete ambaye alikuwa mkoani Tanga
kwa ziara ya kikazi ya wiki moja alihitimisha ziara hiyo jana ambapo pamoja na
mambo mengine alisema kuwa serikali itajenga kivuko kingine kwenye mto huo
chenye uwezo mkubwa zaidi ili kuboresha shughuli za kiuchumi na kijamii
wilayani humo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya
majumuisho wakati akihitisha ziara yake ya kikazi ya wiki moja mkoani Tanga
ambapo alizindua na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo. (Picha zote na Freddy
Maro)
No comments:
Post a Comment