Ni sukari, chumvi, majani ya chai, mchele, sabuni, mafuta, unga wa
sembe, unga wa ngano, juice za matunda na vinginevyo kama sehemu ya
msaada wa chakula toka Airtel Tanzania kwa Kituo cha watoto yatima cha
Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini
Mwanza.
Meneja wa Airtel mkoa wa Mwanza David Wankulu (kushoto) akiwa na Meneja
wa Masoko Kanda Emanuel Raphael wakisaidizana kufanikisha shughuli hiyo
ya makabidhiano.
Meneja Biashara Kanda ya Ziwa Raphael Daudi (wa tatu kutoka kulia)
akiwa na Meneja wa Masoko Kanda Emanuel Raphael (wa kwanza kulia) pamoja
na Meneja wa Airtel mkoa wa Mwanza David Wankulu wakikabidhi msaada wa
chakula cha kufuturisha katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kwa
Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kuendeleza Quran na Suna Tanzania (JUQUSUTA)
Twaha bin Bakari Utari (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha na
wadau wengine wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith
kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza.
Mafuta kwa Kituo.
Vijana wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo
la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza katika picha ya makabidhiano na
wadau wa Airtel.
"Hawa ni watoto wetu, hivyo tunapaswa kuwalinda", Kauli
ya pamoja ya wadau wa Airtel kwa wale wote wenye mapenzi mema.
KAMPUNI Simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa huduma kwa
jamii imeanza kutoa futari katika vituo vinavyolea watoto waliopo katika
mazingira magumu nchini.
Kupitia mpango huu Airtel imetoa msaada wa chakula kwa kituo cha
Sharif Saidi Al-Bath kinacholea watoto yatima kilichopo Nyegezi Majengo
Mapya Jijini Mwanza
Akiongea wakati wa kukabithi msaada huu , Meneja wa Kanda ya Ziwa
wa Airtel Bwana Raphael Daudi alisema” Airtel Kwa kutambua changamoto
nyingi zinazozikumba jamii tumeonelea ni vyema katika mfungo huu wa
ramadhani kutenga muda wa kutembelea na kutoa msaada kwa vituo
mbalimbali vya watoto yatima nchini. Leo tumetembelea kituo hiki cha
Sharif Saidi Al-Bathi na kuwapatia msaada wa chakula ambacho kitawasaidi
hata baada ya mwezi wa Ramadhani.
"Lengo letu ni kuhakikisha tunagusa mahitaji ya jamii kwa ujumla,
husasani watoto kupitia vituo vinavyowatunza huku tukihakikisha
tunarudisha faida tunayoipata kwa kuwafikia watanzania wengi kupitia
shughuli zetu za huduma kwa jamii kila mwaka", alisema.
Kwa upande wake Kiongozi wa Kituo cha Sharif Saidi Al-Bath bwana
Alhaji Hussein Mussa Alisema” Tunawashukuru sana Airtel kwa msaada huu,
tumefurahi sana na kuona kumbe watanzania wenzetu na mashirika
mbalimbali wanaunga mkono jitihada zetu katika kuhakikisha tunawalea na
kuwasomesha watoto yatima. Kituo chetu bado kina mahitaji mengi hivyo
natoa wito kwa taasisi zingine kujiunga na kuendelea kusaidia kituo
chetu na vituo vingine nchini.
Baadhi ya watoto wanaoishi katika kituo hiki wameishukuru Kampuni
ya Airtel kwa msaada wa vitu mbalimbali walivyotoa na kuyatala makampuni
mengine kuiga yale yaliyofanywa na kampuni hiyo.
Vituo vingine vitakavyopata msaada kutoka Airtel ni pamoja na New
Hope Family group-Temeke, Al-Hidaya children’s Home-ilala, Irishad
Madrasah-Mbezi kwa Msuguri (kinondoni), Kiboa orphanage-Arusha na
Heartfelt orphanage care Mbeya, Kituo cha Sharif Saidi Al-Bath chenye watoto Yatima zaidi ya 50
kilichopo Mwanza tayari kimepokea msaada kutoka Airtel mwishoni mwa
wiki.
No comments:
Post a Comment