TANGAZO


Saturday, July 26, 2014

Rais Kikwete atunuku Shahada katika Mahafali ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi jijini Dar es Salaam

 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akimtunuku Luteni Jenerali C.L. Makakala, Shahada ya Uzamili ya Falsafa ya Usalama na Stratejia katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), chuoni hapo, Kunduchi jijini Dar es Salaam leo, Julai 26, 2014. Luteni Jenerali Makakala, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi wa Kwanza, amekuwa
mtunukiwa wa kwanza wa Shahada hiyo, hapo chuoni.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia baada ya kutunuku shahada katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), chuoni hapo, Kunduchi jijini Dar es
Salaam leo, Julai 26, 2014. Jumla ya wahitimu 30, wamehudhuria kozi hiyo, wakiwemo Maofisa Wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine
vya usalama na Idara mbalimbali. Washiriki wengine tisa wametoka  nchi za nje, ambazo ni Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Rwanda, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati), akipiga ya kumbukumbu na wahitimu wa Kozi ya Pili ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC), chuoni hapo, Kunduchi jijini Dar es Salaam leo, Julai 26, 2014.

No comments:

Post a Comment