Waandishi wahabari wakimfuatilia kwa makini Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) mapema hii leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumzia mikakati ya Wizara yake katika kutatua changamoto zinazolikabiri Shirika la Reli laTanzania na Zambia (TAZARA). (Picha zote na Eliphace Marwa-Maelezo)
Na Rose Masaka, SJMC
SHERIA ya uanzishwaji na uendeshaji wa Shirika la
Reli TAZARA kuboreshwa ili kutoa fursa kwa Shirika hilo kujiendesha Kibiashara.
Haya yamebainishwa na
Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania Dkt. Harrison Mwakyembe alipokutana na wandishi
wa Habari leo jijini Dar es Salaam ili kutoa taarifa ya mkutano baina ya
Mawaziri wa Uchukuzi na Fedha kutoka Tanzania na Zambia uliofanyika hivi
karibuni jijini Lusaka nchini Zambia.
Dkt. Mwakyembe alisema
kuwa mpaka sasa Tanzania imekwisha wasilisha mapendekezo ya maboresho ya Sheria
hiyo na kuongeza kuwa kinachosubiriwa ni ni kwa upansde wa Zambia kukamilisha
taribu ambapo watawasilisha marekebisho hayo mwezi ujao.
Aidha Mwakyembe
aliongeza kuwa pamoja na marekebisho hayo ya Sheria washirika wa TAZARA wamefikia
maamuzi ya kuondoa madaraka ya Shirika hilo kutoka Makao Makuu na kuyapeleka
katika ngazi ya Mikoa ambayo ni Tanzania na Zambia.
Kufuatia muundo huo
mpya kila mkoa utashughulika na masuala yote ya ndani kama kusimamia Treni za abiria
na uchukuzi wa mizigo ya ndani ya nchi wakati Makao makuu yatashughulika na
masuala yanayovuka mipaka baina ya nchi hizo mbili.
"Tanzania itaanza na
safari za majaribio kwa muda wa miezi mitatu huku ikifanya safirisha abiria na
mizigo mara mbili kwa wiki ambazo ni siku ya jumanne na ijumaa” Alisema
Mwakyembe.
Wakati huo huo Waziri
Mwakyembe ameongeza kuwa Serikali imekusudia kuanzishwa safari ya Treni maalum
kutoka Makambako kupitia Mlimba – Msolwa hadi Mkamba ili kuondoa adha ya
usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo.
Dkt.Mwakyembe amesema
kuwa Treni hiyo Maalum yenye mabehewa matano ya abiria na behewa la mizigo
itasaidia katika mnaeneo hayo kwakuwa ni jiografia yake ni ya miinuko.
Mkutano wa Mawaziri hao
ulifanyika ikiwa ni desturi ya viongozi wa nchi washirika wa TAZARA, Tanzania
inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano huo
mapema mwezi Agosti .
No comments:
Post a Comment