Askari kanzu (wa pili kulia), akimpeleka kituo cha Polisi cha Kati, kijana aliyedhaniwa kumkwapua mpita njia fedha taslim, zilizotajwa kufikia sh. mil. 5, maeneo ya Mtaa wa Samora, Dar es Salaam juzi, akiwa na wenzake wawili, ambao walifanikiwa kukimbia na fedha hizo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Kijana aliyedhaniwa kumkwapua mpita njia fedha, akivuja damu baada ya kupata kipigo kutoka kwa wapitanjia walioshuhudia tukio hilo. |
Kijana (kulia), akimuomba Askari kanzu awaachie kijana mkwapuaji waweze kumfunza kwa kumtandika ili kijana huyo, akome kukwapua vitu vya watu.
Askari kanzu akiendelea kumpeleka kijana mkwapuaji kwenye Kituo cha Polisi cha Kati baada ya kukataa ombi la kijana aliyetaka awaachie wampige.
Kijana mwingine (kulia), akimuomba Askari kanzu awaachie kijana huyo mkwapuaji waweze kumfunza kwa kumtandika ili kijana huyo, akome kukwapua vitu vya watu.
Kijana (kulia), akiendelea kumshawishi kumuomba Askari kanzu awaachie kijana huyo, mkwapuaji waweze kumfunza kwa kumtandika ili kijana huyo.
Kijana mkwapuaji akimsema kijana aliyekuwa akimshawishi Askari kanzu.
Kijana wa mwanzo akiwa amerudi tena akishirikiana na wa pili (kulia), wakimuomba Askari kanzu awaachie kijana huyo, mkwapuaji waweze kumfunza kwa kumtandika ili kijana huyo, asirudie kukwapua vitu vya watu.
Hapa vijana hao, wakianza kumvamia ili waendelee kumpiga kijana huyo, mkwapuaji.
Askari kanzu akichamaa baada ya kuona vijana hao wanataka kumchukua kwa nguvu.
Hapa vijana waliokuwa wakisaidia kumpeleka kijana huyo, wakimsukuma mkwapuaji ili kwenda kituoni.
Kijana mkwapuaji akisukumwa na Askari kanzu kuelekea Kituo cha Poli cha Kati.
Vijana hao, wakiendelea kumfuata kijana huyo mkwapuaji.
Askari kanzu (kulia), akiwa amemshikilia vizuri kijana huyo mkwapuaji wakati akimpeleka kituo cha Polisi cha Kati.
Hapa kijana huyo, akijikinga kutokana na kipigo alichokuwa akikipata kutoka kwa mmoja wa wasindikizaji.
No comments:
Post a Comment