Serikali ya Israel na wapiganaji wa Hamas wameanza kutekeleza makubaliano ya kusitisha vita kwa masaa 12 katika eneo la Gaza kutokana na maswala ya kibinidaamu.
Hatahivyo Israel imesema kuwa itaendeleza mashambulizi yake kuharibu mahanadaki yanayotumiwa na wapiganaji wa Hamas katika masaa hayo
Awali serikali ya Israel ilikataa makubaaliano ya kusitisha kwa mda mrefu yaliopendekezwa na waziri wa maswala ya kigeni nchini marekani John Kerry .
Bwana Kerry amesema ataendelea kushirikiana na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki Moon ili kuafikiwa makubaliano ya kusitisha vita ya siku saba.
Bwana Ban amesema kuwa vita vinavyoendelea vinaonyesha wazi kwamba hakutakuwa na suluhu ya kijeshi na kwamba uzuiaji wa Gaza ni sharti usitshwe.
Zaidi ya raia mia nane wa palestina wameuawa pamoja na wa Israel zaidi 30.
No comments:
Post a Comment