TANGAZO


Saturday, July 26, 2014

Shuwari Gaza kwa saa 12




Gaza

Wakuu wa afya wa Gaza wanasema kuwa miili zaidi ya 80 imekutikana chini ya vifusi tangu kuanza kipindi cha saa 12 Jumamosi cha kusitisha mapigano.
Wapalestina zaidi ya 900 sasa wameuwawa tangu mapigano ya sasa baina ya Israil na Hamas kuanza.
Waisraili karibu 40 wamekufa, wengi wao wanajeshi.
Wapalestina wa Gaza wametoka mabara-barani kutumia nafasi hiyo ya shuwari.
Mabenki na baadhi ya maduka yamefunguliwa.
Msemaji wa idara ya msaada ya Umoja wa Mataifa, Christopher Gunness, alisema saa 12 hazitoshi kusaidia kila mtu:
"hata kabla ya mapigano ya sasa, kwa vile Gaza imezingirwa, asili-mia-95 ya maji ya bomba hayanyweki.
Katika vituo vya hifadhi 83 tulivyonayo Gaza, ukifungua bomba la maji unapata maji ya chumvi.
Kwa hivo inabidi tupeleke kwa magari maji yote ya kunywa.
Hayo ni maji tu.
Fikiria chakula inachobidi kuwapelekea watu 160,000 magodoro, mablanketi.
Orodha ni ndefu.
Bila shaka tutatumia muda huu lakini hautoshi.
Ndio sababu tunasema kuwa mapigano yasitishwe kabisa, kwa sababu ya wanyonge wa Gaza."

No comments:

Post a Comment