Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Wazara hiyo kuzungumza na kuzindua tovuti ya Kongamano la Kwanza la Ufugaji Nyuki Afrika mwaka 2014 uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julias Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu
akizungumza na hadhiri wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Kwanza la Ufugaji
Nyuki Afrika mwaka 2014 uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa
Julias Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu,
akijisajili kushirikia kwenye tovuti ya Kongamano la Kwanza la Ufugaji Nyuki
Afrika mwaka 2014, kama ishara ya kuzindua tovuti hiyo, shughuli
iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano
wa Kimataifa wa Julias Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Maimuna Tarishi na Msemaji wa Wizara Nurdin Chamuya.
Baadhi ya washiriki wa uzinduzi huo, wakifuatilia uzinduzi wa tovuti hiyo.
Baadhi ya washiriki wa uzinduzi huo, wakifuatilia matukio mbalimbali ya uzinduzi wa tovuti hiyo.
Waziri Nyalandu, akizungumza wakati wa uzinduzi wa tovuti hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Na Hussein
Makame-MAELEZO
WAZIRI wa
Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amewataka wafungaji wa nyuki, wataalamu wa
fani mbalimbali, watafiti, wafanyabiashara na wadau wengine kushiriki Kongamano
la Kwanza la Ufugaji Nyuki Afrika mwaka 2014 litakalofanyika kuanzia Novemba 11
hadi 16 jijini Arusha.
Ametoa wito
huo, wakati akizundua tovuti ya kongamano hilo kwenye ukumbi wa mikutano wa
Kimataifa wa Julias Nyerere jijini Dar es Salaam leo na kuzikumbusha
halmashauri za wilaya nchini ziwawezeshe wafugaji wa nyuki kutoka wilaya zao
washiriki kongamano hilo.
“Wengi
mnaweza kujiuliza kwa nini tunazindua, ni sahihi jibu kuwa:moja tunajivunia kwa
kuandaa tukio muhimu kwa manufaa ya Afrika nzima katika kuendeleza ufugaji nyuki”
alisema Waizari Nyalandu na kuongeza:
“Mbili
tunaitangza Tanzania duniani kote kuwa maliasili tulizonazo yaani misitu na
mapori yanatumika kwa kufuga nyuki; tatu Wizara ya Maliasili na Utalii inaandaa
kongamano hili ili kuhamasisha ufugaji nyuki nchini”
Waziri
Nyalandu alieleza sababu nyingine la kuandaa kongamano hilo ni heshima kwamba
Tanzania inawajali wafugaji nyuki kwa kuwa ni kongamano la kwanza kufanyika
Afrika na Tanzania.
“Nachukua
fursa hii kuwaomba wafugaji nyuki, wataalamu wa fani mbalimbali, watafiti,
waandishi wa habari, wafanyabiashara, wanafunzi na watendaji katika taasisi
mbalimbali kushiriki kongamano hili” alibainisha Waziri Nyalandu.
Naye Katibu
Mkuu wa wizara hiyo Maimuna Tarishi alisema tovuti ya kongamano ambayo ni http://www.apiafrica.org iliandaliwa na
kuanza kutumika Februari mwaka 2014.
Aliongeza
kuwa tuvuti hiyo inawezesha kupata taarifa muhimu za mahali litakapofanyika,
kujiandikisha, kulipia banda la maonesho na ziara ya mafunzo, ambapo hadi sasa
takriban washiriki 550 wakiwemo 250 kutoka nje ya nchi.
Alifafanua
kuwa Wizara yake kwa kuzingatia uzoefu ilionao kwa kushiriki maonesho
mbalimbali, iliona ni vyema kuandaa kongamano hilo ili kushirikisha wadau
mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kutoa mchango wa utafiti, teknolojia na kubadilishana
uzoefu katika kuboresha, kutunza na kusimamia makundi ya nyuki kwa uzalishaji
wenye wingi na ubora.
Kwa mujibu
wa Afisa Nyuki Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Monica Kagya ada ya
ushiriki kwa washiriki kutoka Tanzania ni Shilingi 100,000, mwanafunzi Shilingi 20,000 na mshiriki kutoka nje ya
nchi ni Dola 250.
|
No comments:
Post a Comment