Kamishna Msaidizi wa Madini, Uratibu, Mhandisi John Shija akiwaeleza wanafunzi namna shughuli za uchimbaji madini zinavyofanyika nchini wakati wanafunzi hao walipotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja , Jijini Dar es Salaam.
Mhandisi wa Nishati kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Robert Dule, akiwaeleza wanafunzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu nishati wakati wanafunzi hao walipotembelea banda la Wizara.
Watumishi
wa Wizara ya Nishati na Madini na baadhi ya Watumishi wa Taasisi zilizo chini
yake wakiwa katika picha ya pamoja katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa
Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Na
Asteria Muhozya, Dar es Salaam
BAADHI ya Wanafunzi
kutoka baadhi ya Shule za Sekondari mbalimbali Jijini Dar es Salaam
wametembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zilizo chini yake
kutaka kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na zinazofanyika.
Wakati wanafunzi hao walipotembelea
Wizara na Taasisi zake, wameoneshwa kuvutiwa na kutaka kufahamu kuhusu namna
shughuli za uchimbaji madini nchini zinavyofanyika, kutaka kufahamu aina za
madini yenye thamani kubwa na madini
yenye uzito mkubwa.
Vilevile, wanafunzi
hao wametaka kuelimishwa kuhusu shughuli za utafiti na uchimbaji wa gesi
zinazofanyika nchini ikiwa ni pamoja na kutaka kufahamu vyuo mbalimbali
vinavyotoa mafunzo kuhusu masuala ya gesi, mafuta na madini.
Aidha, wengi wao walipenda
kuona madini ghafi ya Tanzanite yanayopatikana nchini ikiwa ni pamoja na
kufahamu aina zote za madini yaliyopo chini. Wanafunzi hao wamepata nafasi ya
kupata majibu kuhusu masuala mbalimbali waliyouliza kutoka kwa waatalamu
mbalimbali wa Wizara na Taasisi waliopo katika maonesho hayo.
|
No comments:
Post a Comment