TANGAZO


Thursday, June 19, 2014

Waandishi wa habari watakiwa kujifua Kiingereza ili wawe na ufanisi kikazi



Ofisa Miradi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia wahamaji na wahamiaji (I O M), Charles Mkude akiwafundisha waandishi wa habari wa Dodoma kwa kutumia michoro wakati wa mafunzo ya namna ya kuandika habari zinazowahusu wahamiaji yaliyofanyika kwa siku tatu. (Picha zote na John Banda)

Ofisa Makazi (Hifadhi) wa Shirika la Kimataifa la wakimbizi (UNHCR), Nicholaus Gichubiri akisisitiza jambo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma walioitwa kupewa mafunzo ya jinsi ya kuandika habari za wakimbizi.
 Ofisa Makazi (Hifadhi) wa Shirika la wakimbizi, Nicholas Gichubiri akijiandaa kujibu maswali ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma wakati wa mafunzo kuhusu uandishi wa habari za wakimbizi yaliyofanyika kwa siku tatu mjini humo.

Waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Mashirika ya Kimataifa yanayoshughulikia Wakimbizi ya I O M na UNHCR, mara baada ya mafunzo ya siku tatu yaliyolenga uandishi wahabari za wakimbizi.

Na John Banda, Dodoma

WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuwa na uelewa wa kutosha katika lugha ya kiingeleza ili iwe rahisi katika utendaji wa kazi zao za kila siku.

Hayo yalisemwa na Ofsa Miradi wa Sharika la Kimataifa la wahamiaji na wahamaji [I O M] Charles Mkude wakati alipokuwa akihitimisha mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa Habari mkoani Dodoma.

Mkude alisema Kiingereza ndiyo Lugha pekee inayounganisha ulimwengu na walimwengu katika mawasiliano na kufanya mwandishi kuandika kwa usahihi.

Alisema wengi wa waandishi wa habari hapa nchini wameshindwa kuitendea haki taaruma yao kutokana na kuwa na uelewa mdogo wa Lugha hiyo hasa linapofika swala la kufanya uwiano wa habari kutoka kwa wahusika hasa kama wakiwa hawajui Kiswahili.

Ofisa huyo wa I O M alibinisha kuwa ni vigumu kukuta taarifa mbalimbali zinazohusu wahamiaji ambao wamekuwa wakikamatwa na maofisa uhamiaji wakiwa wamehojiwa na kusema mashwahibu yaliyowakumba walikotoka badala yake huandikwa upande mmoja.

‘’Lichukueni hili la Lugha ya kiingereza ambayo itawarahisishia katika utendaji wenu wa kazi kama changamoto ya kuifanyia kazi kwa sababu hata hapa nchini tunatumia vitu vilivyoandikwa kwa lugha hiyo mfano Toothpick yaani vimbata vya kuchokonolelea Meno’’, alisema.

Aidha alisema makundi mbalimbali wakiwemo maofisa uhamiaji na polisi ambapo wao wamekuwa wakifanya nao mafunzo mbalimbali.

Shirika hilo limekuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo kwa makundi mbalimbali hasa yanayojihusisha na wahamiaji, wahamaji pamoja na biashara haramu ya Binadamu wanaoingia nchini wakikimbia kwenye nchi zao kutokana na sababu mbalimbali, wakishiriki pamoja na UNHCR.

No comments:

Post a Comment