Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa
China Li Yunchao ukiwasili katika Viwanja vya Ofisi za Shirika la Taifa la
Utangazaji (TBC) alipotembelea kwa ajili ya hafla ya Kukabidhi na kuzindua gari
la kurushia matangazo (OB Van) lililotolewa kwa Msaada wa Serikali ya China
jana jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li
Yunchao akisalimiana na baadhi ya Wafanyakazi wa Startimes na TBC mara baada ya
kuwasili katika Viwanja vya Ofisi za Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC)
alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya Kukabidhi na kuzindua gari la kurushia
matangazo (OB Van) leo jijini Dar es Salaam.Gari hilo limetolewa kwa Msaada wa
Serikali ya China.Katikati ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa
Tanzania Dkt. Fenella Mukangara.Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akijadiliana na jambp na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, katikati ni Mwakilishi wa Kampuni ya Startimes Bw. Jack Zhou.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (katikati) wakati wa hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa Gari la kisasa la kurushia matangazo ya moja kwa moja (OB Van) ambalo Serikali ya China ili kutoa msaada kwa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC). Kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Bw. Clement Mshana.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akitoa hotuba wakati wa hafla fupi ya makabidhiano na uzinduzi wa gari la kurushia matangazo(OB Van) la Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) leo katika viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (wa pili kutoka kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya Gari la kurushia matangazo la TBC, kutoka kulia ni Makamu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya watu wa China Li Jingzao, Makamu wa Rais wa China Li Yunchao na wa mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Bw. Clement Mshana.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara( wa pili kutoka kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya Gari la kurushia matangazo la TBC, kutoka kulia ni Makamu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya watu wa China Li Jingzao, Makamu wa Rais wa China Li Yunchao na wa mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Bw. Clement Mshana.
Gari la kisasa la kurushia matangazo ya moja kwa
moja lililokabidhiwa kwa TBC likiwa katika viwanja vya Shirika hilo Mikocheni
jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akikagua ndani ya Gari la kisasa la kurushia matangazo la TBC mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam.
Pichani baadhi ya Screen zikionyesha picha mbalimbali za matukio yaliyokuwa yakirushwa moja kwa moja wakati wa hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa Gari la kisasa la kurushia matangazo la TBC lililopatikana kwa msaada wa Serikali ya China.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt.
Fenella Mukangara akikabidhiwa mfano wa Ufunguo wa gari la kurushia matangazo
la TBC mara baada ya kuzinduliwa leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Waziri wa
Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China Li Jingzao.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi mfano wa Ufunguo wa gari la kurushia
matangazo Mkurugenzi Mtendaji wa TBC Bw. Clement Mshana mara baada ya gari hilo
kukabidhiwa na kuzinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt.
Fenella Mukangara akimkabidhi zawadi ya Kinyago cha mnyama Twiga Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao mara baada ya kuzindua gari la kurushia
matangazo la TBC leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Clement
Mshana.
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Utawala Bora Kapteni George Mkuchika na Mkurugenzi Mtendaji wa TBC Clement
Mshana wakifuatilia mazungumzo baina ya Makumu wa Rais wa China Li Yunchao na
Mwakilishi wa Startime (hawapo pichani) alipotembelea ofisi za Kampuni hiyo jana,
jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li
Yunchao akiangalia picha zinazoonyesha vipindi vinavyorushwa na Startimes
alipotembelea ofisi za Kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
Katikati Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiwa na mgeni wake, Makamu wa Rais wa China Li Yunchao kushoto kwa Waziri Fenella katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali na wafanyakazi wa TBC na Startimes. (Picha zote na Frank Shija. WHVUM)
No comments:
Post a Comment