*Kuuzwa Kielektroniki
*Ni kupitia huduma ya M pesa*Watu wazima kulipa 2500/- kwa siku na watoto 500/-
*Tiketi za kupaki magari madogo kwa siku ni 4000/- maroli ni 40000/-
Meneja bidhaa na Maendeleo ya M-Pesa wa Vodacom Tanzania, Moses Krom akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusiana na kulipia viingilio kwa njia ya M-Pesa katika maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba)Dar es Salaam yatakayo anza rasmi kesho na kumalizika julai 8 mwaka huu. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Anna Bulando.

Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Anna akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) kuhusiana na kulipia viingilio kwa njia ya M-Pesa na usalama katika
maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba)Dar es Salaam yatakayo anza
rasmi kesho na kumalizika julai 8 mwaka huu. Kulia ni Meneja bidhaa na Maendeleo ya M-Pesa wa Vodacom
Tanzania, Moses Krom.
Dar es salaam 27 juni 2014,
MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), imetangaza viingilio vipya vya watu na magari katika maonesho ya
kimataifa ya Dar es salaam, (DITF) yatakayo anza tarehe 28 ya mwezi juni hadi
tarehe 8 mwezi Julai.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Bi. Anna Florence
Bulondo amesema viingilio vya mwaka huu havina tofauti na vya mwaka jana lakini
sasa yamefanyika maboresho ikiwa ni pamoja na ukataji wa tiketi kwa njia ya
Kielectroniki na kwa njia ya M -pesa.
“Viingilio
vya mwaka huu ni Shilingi elfu 2500 kwa watu mzima na shillingi 500 kwa watoto
kila siku isipokuwa siku maalum ya tarehe 7 ambapo viingiio vitakuwa shilingi
3000 kwa watu wazima na watoto shilingi 1000.” Alisema Bulondo.
“Kwa
watakao hudhuria maonyesho hayo na magari madogo watatakiwa kununua tiketi kwa
shilingi 4000, kama ambavyo mchanganuo wa malipo unavyobainisha malipo ya
huduma nyingine zikiwemo za kupaki magari kama malori na magari makubwa pamoja
na huduma nyingine.”
Aidha,
Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo aliongeza kuwa, katika maonesho ya Mwaka huu,
Usalama umeimarishwa kwa kiasi kikubwa na kutakuwa na Ulinzi wa Uhakika pamoja
na Camera maalum zitakazo wekwa katika mageti na sehemu mbalimbali kuzunguka
maeneo yote ya maonesho.
Kwa
Upande wake, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin
Twissa, amesema kwa mwaka wa pili sasa wameendelea kuwawezesha watu, kufanya
malipo ya tiketi kwa njia ya M pesa.
“M
pesa inaendelea kurahisisha maisha ya Watanzania na mwaka huu, watu wote
watakao kuja katika maonesho haya tumewawezesha kulipa viingilio kupitia M pesa
na pia kufanya manunuzi na kulipa kwa M pesa katika banda letu la Vodacom.”
Alisema Twissa.
Malipo
ya ada binafsi.
1.
Kwa siku - watu wazima (siku za
kawaida) – 2,500/-
2.
Kwa siku- watoto (siku za kawaida) –
500/-
3.
Kwa siku – watu wazima (siku ya
SabaSaba) – 3,000/-
4.
kwa siku – Watoto (siku ya SabaSaba) –
1,000/-
5.
malipo kwa kipindi chote cha maonyesho
- Beji kwa wahusika wa maonyesho -
20,000/-
6. Beji
kwa wahusika wa maonyesho (maeneo) – 3,000/-
Tiketi
za uegeshaji magari.
1.
Kwa siku (magari madogo) -
4,000/-
2.
kwa kipindi chote cha maonyesho –
30,000/-
3.
Malipo kwa pamoja – 200,000/-
4.
Tiketi za maegesho maalum – 400,000/-
5.
Maroli na magari makubwa – 500,000/-
6. Malipo
ya kuegesha magari nje ya viwanja vya saba saba – 1,500/-
Maonesho
ya kimataifa ya Dar es salaam ni maonesho pekee yanayoongoza katika huduma za
masoko Tanzania, maonesho hayo yanayodumu kwa siku kumi, huvutia watazamaji
zaidi ya laki tatu na nusu na kutoa fursa kwa makampuni kuonyesha bidhaa zao na
wanaohudhuria kununua vitu mbalimbali kwa gharama nafuu na kupata fursa ya
kuuliza maswali na kulinganisha ubora wa bidhaaa kadha wa kadha.
No comments:
Post a Comment