*Kiingilio
ni kama mwaka jana, Banda maalumu kuitangaza Tanzania
*Nchi
31 kushiriki, zipo pia Wizara na Taasisi za Serikali, Mashirika na Makapuni
binafsi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashra Tanzania (TanTrade), Bi. Jacqueline Maleko.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashra Tanzania (TanTrade), Bi. Jacqueline Maleko.
Na
Johary Kachwamba- MAELEZO
Maonesho
ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam (38th DITF)
yanatarajia kuanza tarehe 28 mwezi huu
na kufikia kilele chake tarehe 8 Julai 2014 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K.
Nyerere, barabara ya kilwa, jijini Dar-es-salaam.
Akitoa
taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bibi. Jacqueline Mneney Maleko imeeleza kuwa maonesho ya
mwaka huu yataongozwa na kauli mbiu isemayo “Tunaunganisha Uzalishaji na Masoko”
Amesema
kuwa Kauli Mbiu hiyo imechaguliwa kutumika kuonesha uhusiano uliopo kati ya
Uzalishaji na Masoko na umuhimu wa
mnyororo wa uzalishaji ambao ndio chimbuko la upatikanaji wa Bidhaa bora zenye
ushindani katika soko.
Bibi.
Maleko amesema kuwa mwaka huu TanTrade imetenga eneo kubwa zaidi kwa ajili ya
Wazalishaji wa ndani ya nchi na kubainisha maeneo yatakayotumiwa na wazalishaji
hao kuwa ni jengo namba C.19 na eneo la wazi lililo nyuma ya ofisi za
Mkurugenzi wa Utafiti, Mipango na Uwezeshaji kwa ajili ya bidhaa za kilimo na
bidhaa zinazotengenezwa Tanzania.
Kuhusu
ushiriki wa mataifa mengine katika maonesho hayo amefafanua kuwa tayari nchi 31
zimethibitisha kushiriki maonesho hayo zikiwemo Afrika Kusini,Czech Republic,
China, Ghana, Indonesia, India, Iran, Finland, Ugiriki, Italia, Japan, Jordan,
Kenya, Korea ya Kusini, Malaysia, Marekani, Misri, na Ujerumani.
Nchi
zingine ni pamoja na Nigeria, Pakstani, Rwanda, Saudi Arabia, Singapore,
Sudani, Syria, Uganda, Uingereza, Burundi, Sweden, Vietnam na Zimbabwe.
Aidha,
amefafanua kuwa makampuni ya nje 490 yamethibitisha kushiriki katika maonesho
hayo huku Wizara na Taasisi za Serikali
zilizothibitisha kushiriki maonesho hayo zikifikia 61.
Kwa
upande wa Mikoa amesema tayari mikoa 10 imethibitisha kushiriki ikiwemo, Mikoa
ya Iringa, Ruvuma, Mbeya, Pwani, Kigoma, Kagera, Geita, Mara, Manyara na
Ruvuma. Jumla ya Washiriki waliothibitisha kushiriki kutoka ndani ya nchi ni
1700.
Kuhusu kiingilio wakati wa maonesho hayo amesema
watu wazima walipia Shilingi 2,500 na
watoto ni 500 kila siku kwa siku zote za maonesho isipokuwa tarehe 7 Julai,2014
ambapo ada itakuwa Shs. 3,000/= kwa watu wazima
na watoto ni Shs.1000/=
No comments:
Post a Comment