Mfuko wa Fursa Sawa kwa
Wote (EOTF) utaendesha Semina ya mafunzo ya siku 3 kwa Wanawake Wajasiriamali
itakayofanyika kuanzia tarehe 23 hadi tarehe 25 Juni 2014, kuanzia saa 2 asubuhi
katika ukumbi wa JKT Mgulani, Temeke,jijini Dar es salaam.
Lengo la mafunzo haya
kwa mwaka huu ni kuwaelimisha wanawake jinsi ya kupata mitaji kwa ajili ya
biashara, masoko pamoja na stadi za ujasiriamari.
Katika semina hii mada
kuu zitahusu Uwekezaji na Ukuzaji mtaji, Utunzaji wa Kumbukumbu za Biashara kwa
Kutumia Mashine za EFD, Kuwaunganisha Wazalishaji na Masoko, Mbinu za kushiriki
Maonesho ya Biashara, Utaalamu wa kusindika Mazao, Usajili na Matumizi ya “Bar
Code” na nyinginezo.
Aidha, elimu juu ya
maradhi sugu yanayorudisha nyuma maendeleo ya wanawake itatolewa na jinsi ya
kujikinga dhidi ya Malaria, Dengue, Saratani ya Matiti na Shingo ya Uzazi
pamoja na Fistula.
Watoa mada katika
semina hii ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa IPP Dkt. Reginald Mengi, Wakufunzi
kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Soko la Hisa la Dar-es-salaam- DSE,
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara-TanTrade na Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam.
Pia kutakuwa na Madaktari
kutoka Manispaa za Ilala na Temeke, hospitali ya Ocean Road na CCBRT.
Natumia fursa hii adimu
kuhamasisha wanawake kuudhuria Semina hii muhimu yenye lengo la kuwajengea uwezo
wanawake na vijana wajasiriamali na kuwainua kiuchumi kwa siku zote 3 kuanzia
tarehe 23 hadi 25, Juni 2014.
Hakuna malipo kwa
washiriki
Imetolewa
na Mkurugenzi Mtendaji,
Mfuko
wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF).
Ndugu,
Stephen Emmanuel
20/06/2014
No comments:
Post a Comment