Baadhi ya wananchi wakifuatilia maelezo kutoka kwa Wafanyakazi wa TASAF wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

Ofisa Mifumo wa TASAF Bi. Desderia Bomba –Misaakitoa maelezo kuhusu Miradi inayotekelezwa na TASAF Awamu ya Tatu kwa mwananchi aliyetembelea banda lao wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,mwenye fulana nyeupe kushoto ni Mfanyakazi wa Mapokezi wa TASAF Bi. Jenny Solomon
Mtaalam Msaidizi wa Uchapishaji Bw. Victor Manyai akimkabidhi baadhi ya machapisho ya TASAF mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la TASAF katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mfanyakazi wa Mapokezi wa TASAF Bi. Jenny Solomon.
Kutoka kushoto ni Afisa Mawasiliano wa TASAF Bw. Zablon Bugingo, , Afisa Mifumo, Bi. Desderia Bomba –Misa, Mtaalam wa Mawasiliano, Bibi. Zuhura Mdungi, Afisa Mapokezi Bi. Jenny Solomon na Mtaalam Msaidizi wa Uchapishaji Bw. Victor Manyai wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya banda lao wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Mpima Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Edwin Emmillian akimuelekeza Mwanafunzi wa Kidato cha Pili Shule ya Sekondari Benjamini alipotembelea banda la Wizara hiyo wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Frank Shija, WHVUM)
No comments:
Post a Comment