Flashback:
Hayati Baba wa Taifa enzi za uhai wake akiingia katika Kanisa la
Mtakatifu Peter la Oysterbay jijini Dar es salaam. Alifanya hivyo kila
siku asubuhi
Baadhi
ya Watanzania wakati Rais wa Uganda, Mhe Yoweri Kaguta Museveni
akiwatubia mamia ya wananchi waliohudhuria misa ya kuombea mchakato wa
kumfanya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kutangazwa Mwenyeheri na hatimaye mtakatifu
Rais
wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiwatubia mamia ya wananchi
waliohudhuria misa ya kuombea mchakato wa kumfanya Baba wa Taifa Mwalimu
Nyerere kutangazwa Mwenyeheri na hatimaye mtakatifu
Baadhi ya watu waliohudhuria walikwenda kumpa mkono Mama Maria Nyerere.
Flashback: January 21, 2006 - Bodi ya Dayosisi ya iliyoundwa kuanza mchakato wa Mwalimu Nyerere kutangazwa Mwenyeheri na hatimaye Mtakatifu.
Na Paul Mallimbo, Kampala, Uganda
Rais
Yoweri Museveni, amesema kiongozi bora ni yule anayefuata maagizo ya
Mungu na kuwatumikia binadamu wote kwa usawa na haki. Rais Museveni
aliyasema hayo (Juni mosi) wakati ibada ya kuombea mchakato wa kumfanya
Marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuwa mwenyeheri na
hatimaye kutangazwa mtakatifu.
Alisema
hata kwenye maandiko matakatifu ya Biblia kuna mistari inayomtaka
binadamu ampende binadamu mwenzake kama anavyojipenda yeye;“Kwenye
biblia kuna sehemu inauliza kuwa utampendaje Mungu ambaye hujawahi
kumuona, na ushindwe kumpenda binadamu mwenzako,” Alisema kwa sababu
aliwahi kufanya kazi na mwalimu, anaweza kutoa ushahidi kwamba mwalimu
alifanya yote mawili, kumtii Mungu na kuwatumikia binadamu.
Alisema
mojawapo ya sababu iliyomfanya Marehemu Papa Paulo II kutangazwa
mtakatifu kuisaidia Ulaya Mashariki, ambayo wananchi wake walikuwa
hawamwamini Mungu. “Marehemu Papa Paulo II alisaidia kuikomboa Ulaya
Mashariki kutoka kwenye ukomunisti, wananchi walikuwa hawaamini kuna
mungu, lakini kwa juhudi zake aliwafanya wamwamini na kumpenda
Mungu,”alisema.
Rais
Museveni alisema anatarajia kupeleka ushahidi kwa Papa Benedict kwamba
Mwalimu anasifa za kutangazwa kuwa mtakatifu kwa sababu alimtii Mungu na
kuwatumikia binadamu. “Mimi nitapeleka ushahidi kwa Papa, kwamba mbali
na mwalimu kumtii Mungu na kuwpenda binadamu wote, pia aliwakomboa
Waafrika kutoka Ruvuma mpaka Capetown, huu ni ukweli siyo
hadithi,alisisitiza Rais Museveni.
Kufuatia
hatua hiyo ya kwenda Roma kutoa ushahidi, Rais Museveni amesema katika
maadhimisho ya kuombea mchakato wa Mwalimu kuwa Mtakatifu
yatakayofanyika mwakani, ameahidi kuwaita maraisi wote waliowahi kufanya
kazi na Mwalimu Nyerere ili kuuthibitishia ulimwengu kuwa Marehemu Baba
wa Taifa ameweza kuwaunganisha Waafrika.
Alifafanua
kuwa Mwalimu ametoa mchango mkubwa wa ukombozi kwa nchi za Msumbiji,
Zambia, Zimbabwe, Namibia, Angola, Afrika Kusini, Uganda na Tanzania
yenyewe. Hivyo kuja kwa viongozi hao kushiriki ibada hii itakuwa Baraka
kubwa.
Rais
Museveni ambaye alitumia muda mwingi wa hotuba yake kuzungumza
Kiswahili, alisema baada ya jitihada za mwalimu kuikomboa Uganda, ndipo
na wao walipoweza kuzisaidia nchi za Rwanda, Sudan Kusini na Congo
kujikomboa na kuongeza kuwa kama si juhudi za mwalimu wasingekuwa na
uwezo wa kuwasaidia wengine.
Aidha
Rais huyo wa Uganda ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986, alisema
kuwa, kwa upande wa viongozi weusi, hakuna kiongozi ambaye ametoa
mchango mkubwa kama Marehemu Mwalimu Nyerere.
“Hapa
Duniani sidhani kama kuna mtu mweusi mwingine ambaye ametoa mchango kama
mwalimu, na hili nimelishudia mwenyewe sikuambiwa na mtu, aliongeza
kuwa, hata mzee wetu Nelson Mandela alifanya kazi kubwa Afrika ya Kusini
lakini Mwalimu alifanya kazi kubwa zaidi ya ukombozi wa Afrika,
Alisema.
Alisema
Mwalimu aliikomboa Tanzania na kuwafundisha dini ya Kristu, kwa vitendo
siyo kwa maneno. Aliongeza kuwa nchi nyingine za Afrika zimepatwa na
machafuko ya ukabila na dini kutokana na msingi mbaya wa viongozi
waliotangulia. “Tanzania
ni nchi ya Wakristo, Waislamu na wale wengine wanaoamini dini za
kienyeji lakini mwalimu aliwafundisha Watanzania fikra za kizalendo za
umoja,alisema .
Alisema
Uganda haikupata elimu nzuri juu ya jambo hilo, viongozi wa kwanza wa
taifa hilo waliwapandikiza wananchi chuki, kwamba dini ni kumchukia
mwenzako, waumini wa dini moja kuwachukkia waumini ya dini dini nyingine
na matokeo yake ni umwagaji wa damu.
“Biblia
inasema kile unachopanda ndicho unachovuna, kwa hiyo sisi hapa
tulipanda mbegu mbaya na tukavuna umwagaji wa damu,” alisema na kuongeza
kuwa Tanzania haijawahi kuona umwagaji mkubwa wa damu zaidi ya ajali za
magari na ile ya kipindi kile wakati askari wa Tanzania walipokwenda
Uganda kupigana na Idd Amin.
Nadhani hii ndiyo damu pekee mmeona,” alisema.
Alisema
baadhi ya waasisi wa Uganda waliwafundisha kuwa wakristu kuwachukia
Waislamu, matokeo yake nchi imekuwa katika umwagaji wa damu tangu
ilipopata uhuru. Aliongeza kuwa mpaka 1986 wakati anaingia madarakani
raia 800,000 wa Uganda walikuwa wamekufa kutokana na chuki za udini na
ukabila.
“Uganda
imeshuhudia umwagaji mkubwa sana wa damu, Congo wameona damu, Sudan,
Somalia, Kenya, Rwanda na Burundi ni Tanzania pekee ambayo imekuwa kama
kisiwa cha amani, hii yote ni kutokana na mchango wa mwalimu Nyerere
ambaye alidumisha amani, umoja na maendeleo kwa watu wake.
Alisisitiza
kuwa, kwa sababu mojawapo ya sababu ya kumfanya mtu awe mtakatifu ni
watu kutoa ushahidi wa matukio mbali mbali yaliyofanywa na mtu huyo
wakati wa uhai wake, aliahidi kwenda Roma kutoa ushahidi kuhusu matendo
ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
“Nikienda
kwa Baba Mtakatifu, Papa Benedict nitatoa ushahidi mzuri juu ya
marehemu Mwalimu Nyerere tena nitatoa kwa maandishi siyo kwa maneno
pekee yake”alisisitiza.
Ibada
ya kumuombea Baba wa Taifa ilifanyika katika Kanisa la Mashahidi wa
Uganda, Namugongo, ambapo ibada hiyo iliendeshwa na Askofu Mkuu wa Jimbo
la Kampala, Dk. Cyprian Kizito Lwanga, ambaye aliiomba serikali
kusaidia kuboresha eneo la kanisa hilo ili liwe na miundombinu ya kisasa
zaidi.
Hii ni
mara ya nane ibada ya kuombea mchakato wa kumfanya baba wa Taifa kuwa
Mwenyeheri na hatimye mtakatifu unafanyika katika kanisa hilo nchini
Uganda. Mchakato huo ulianza mwaka 2006.
Katika
ibada hiyo ambayo imehudhuria na maelfu ya Watanzania, pamoja na
mataifa mbali mbali duniani, pia ilihudhuriwa na familia ya Marehemu
Baba wa Taifa, Waziri Mkuu wa Uganda Amama Mbabazi mawaziri na wabunge
kutoka Uganda, ambapo Tanzania iliwakilishwa na Balozi wa Tanzania
nchini Uganda.
No comments:
Post a Comment