Utafiti uliofanywa na shirika
moja la misaada Uingereza umeonyesha kuwa ubakaji unatumiwa tena kwa
kiasi kikubwa gerezani kama adhabu kwa wanawake wanaojihusisha na
masuala ya siasa nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.
Utafiti huo uliofanywa na "Freedom from Torture"
umegundua kuwa zaidi ya nusu ya wanawake wote walio fanyiwa uchunguzi
walikuwa wamebakwa na magenge.Wanawake hao waliofanyiwa uchunguzi wanajumuisha wachuuzi, wasomi na hata wataalamu mbali mbali kati ya miaka 18 na 62 kote nchini humo.
Takriban hao wote walitiwa nguvuni kwa kujihusisha na masuala ya haki za binadamu au kampeini za kisiasa, au hata jamaa katika familia yao alihusika na siasa.
Zaidi ya nusu ya wanawake hao wanasema wamebakwa na magenge hata wanaofika kumi. Shirika hilo sasa linataka serikali ya DRC kufanya hima kutekeleza azimio la umoja wa mataifa dhidi ya kuwatesa watu.
No comments:
Post a Comment