Wananchi
wa Kijiji cha Kitwai A, wakiwa wamenyoosha mikono juu, kwenye mkutano wa
hadhara, wakati Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana alipokuwa akimuunga mkono
jambo Mbunge wa jimbo la Simanjiro, Mhe. Christopher Ole Sendeka, katika
suala zima la Utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Katibu
Mkuu wa CCM, ndugu Abdulrahman Kinana akizindua gari la mradi wa
Kukodisha la Kikunndi cha Vicoba Mkombozi chenye wanachama wapatao
30, mjini Orkesument, Wilayani Simanjiro mkoani Manayara.
Kinana
ameambatana
na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, wako moani Manyara kwa
ziara ya siku saba ya Kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo
inayotekelezwa kwa
kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za
mitaa, kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.
Mbunge wa jimbo la Simanjiro, Mhe. Christopher Ole Sendeka, akiwahutubia baadhi ya Wananchi
wa Kijiji cha Kitwai A, akiwa ameambatana na msafar wa Katibu Mkuu wa
CCM, ndugu Kinana, Katika kijiji hicho, ndugu Kinana alizindua Ofisi ya
Mtendaji Kata ya CCM Kitwai A, na kuahidi kujenga shule ya Sekondari kwa
ajili wananchi hao ambao hapo awali walikuwa na shule za msingi tu.
Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Abdulrahman
Kinana akipata maelezo mafupi kutoka
kwa Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, Mhe. Ole Sendeka wakati akiangalia josho
la ng'ombe la Orkirung'rung ambapo kuna mradi wa ufugaji wa ng'ombe chotara
ambao ni ufugaji wenye tija na unasaidia sana kuongeza thamani mifugo.
Mbunge
wa Jimbo la Simanjiro, Mhe. Ole Sendeka akifafanua jambo Kwa Katibu Mkuu
wa CCM, ndugu Kinana (hayupo pichani) kuhuasiana na Mradi huo wa ufugaji wa ng'ombe wa kisasa
(nyama na Maziwa), wakati akiangalia josho
la ng'ombe la Orkirung'rung ambapo kuna mradi wa ufugaji wa ng'ombe
chotara,ufugaji wenye tija na unaosaidia kuongeza thamani mifugo.
Pichani
mbele ye bango kulia ni jengo la Mama na Mtoto la kituo cha Afya
Orkesument, Wilayani Simanjiro, ambalo pia Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana
alikagua.
Katibu
Mkuu wa CCM, ndugu Kinana akimsikiliza Dkt. Juma Nahonyo wakati wa
ukaguzi wa jengo litakalokuwa bohari ya Dawa katika kituo cha Afya cha
Orkesument, kulia ni Mbunge wa jimbo la Simanjiro, Mhe. Christopher Ole Sendeka.
Katibu
Mkuu wa CCM, ndugu Abdulrahman Kinana akizindua mradi wa Kikundi cha
Mazingira kilichopo mjini Orkesument, Wilayani Simanjiro mkoani
Manayara. Kikundi hicho kitatumika kueleimisha wananchi wa mji huo katika
masuala ya usafi na kulinda mazingira, kuwaelimisha wananchi kuhusiana
na mambo ya maambukizi ya UKIMWI,masuala ya Rushwa na mengineyo.
Katibu
Mkuu wa CCM, ndugu Kinana akiwahutubia wananchi wa Orkesument kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika mjini humo wilayani Simanjiro, Kinana
aliwaeleza wananchi hao kuwa ahadi za Rais zilizoahidiwa 2010
zitatekelezwa kwa zilivyoahidiwa kwa wananchi wa Simanjiro, pia
aliwasisitizia wananchi hao kutochagua viongozi wa vijiji wa hovyo ambao
mwisho wa siku ndio wanaoleta mikorogo na migongano kwa wananchi kwa
kuuza ardhi, hali inayoleta migogolo isiyokwisha kila siku.
Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana wakielekea kukagua jengo la Ofisi ya Mtendaji Kata ya CCM Kitwai A, wilayani Simanjiro. |
Mbunge wa jimbo la Simanjiro, Mhe. Christopher Ole Sendeka akitetea jambo na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye katika kijiji cha Kitwai A, Simanjiro mkoani Manyara. |
Mdau akifuatilia jambo, wakati wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana akipokelewa na Mwenyekiti CCM, wilayani ya Simanjiro, ndugu Brown Ole Suya pamoja na Mbunge Mbunge wa jimbo la Simanjiro, Mhe. Christopher Ole Sendeka. |
Jengo la Ofisi ya Mtendaji Kata ya CCM Kitwai A, wilayani Simanjiro lililozinduliwa na Katibu Mkuu wa CCM, ndugu Kinana. |
No comments:
Post a Comment