Waziri
wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza na wageni waalikwa
wakati wa uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya bure kwa waandishi wa habari
kwenye maeneo matano, ambayo ni katika Sekta ya uchimbaji, unyanyasaji wa kjinsia,
kupamba na biashara ya madawa ya kulevya na kuzuia utumiaji wa madawa ya
Kulevya kwa waandishi wa habari na utayarishaji na utengenezaji wa
vipindi vya luninga na wanawake watangazaji jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa juma. Kushoto kwake ni Msaidizi wa Mwakilishi wa Mfuko wa
Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu, Dorothy Temu –Usiri na Mkurugenzi wa
Mfuko wa vyombo vya habari, Ernest Sungura.
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
WAANDISHI
WA HABARI nchini wamehimizwa kushirikiana kwa karibu na Mfuko wa Vyombo
vya Habari (TMF) ili kuacha kutegemea zaidi matangazo kwa sababu kuna
weka taaluma yao rehani.
Akizungumza
na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa kutoa mafunzo kwa
waandishi wa habari jinsi ya kuripoti mambo ya sekta ya uchimbaji,
unyanyasaji wa kijinsia, kupamba na biashara ya madawa ya kulevya na
kuzuia utumiaji wa madawa ya Kulevya na watayarishaji wa vipindi vya
luninga, Waziri wa kazi na Ajira, Mhe, Gaudensia Kabaka amesema kwamba
vyombo vya habari lazima vishirikiane na mfuko huo ili kuwa huru wakati
wa kuripoti.
“kuendelea
kutengemea matangazo kutoka kwenye makampuni mbalimbali ili kujiendesha
kuna wafanya kutokuwa huru katika uandishi wetu na tasnia ya habari kwa
ujumla,” amesema Kabaka
Amesema
mradi huo wa mafunzo ya bure kwa waandishi ni muhimu kwa taifa kwa
sababu tatizo kubwa la ajira hasa kwa vijana na wanawake linachangia kwa
kiasi kikubwa vijana wengi kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za
kulevya.
Baadhi ya wadau na wageni waalikwa wakimsikiliza mgeni rasmi hayupo pichani. Kabaka
aliongeza kuwa mafunzo haya yatakayotolewa kwa ufadhili wa TMF ni
muhimu ili kuelimisha jamii madhara ya kuuza na kusambaza dawa za
kulevya na matumizi yake yanavyoathiri kizazi na kizazi.
“kwa
sasa nchi yetu ya Tanzania ni moja ya nchi zilizoathirika sana na
matumizi ya dawa za kulevya na mbaya zaidi kutumika katika njia ya
kusambaza madawa hayo hatari,”
“kwa
mujibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii tuna jumla ya watu 20,626
walioathirika na dawa za kulevya na kwa sasa wanapatiwa matibabu,”
alisisitiza Kabaka.
Amesema
nchini matumizi ya dawa za kulevya kwa zaidi ni Bangi, Heroin, Mirungi
na Cocaine na cha kutisha matumizi haya yanaathiri pia wanafunzi wa
sekondari na shule za msingi nchini.
Msaidizi
wa Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu(UNFPA),
Dorothy Temu Usiri akitoa nasaha zake kwenye uzinduzi huo uliofanyika
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
Kwa
upande wake, Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa
wa Idadi ya watu, Dorothy Temu-Usiri amesema kuwa kuongezeka kwa vitendo
vya kikatili vya kijinsia na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi
vimechochea kushirikiana na TMF kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari
hapa nchini.
“kwa
kuanzisha mafunzo haya ya bure kutasaidia waandishi wa habari kuandika
kwa kina juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya ambazo ndio
kichocheo cha ukatili wa kijinsia hasa kwa Wanawake,” amesema Usiri
Usiri
aliongeza kwamba nchini Tanzania idadi kubwa ya watu wenye nguvu ya
kufanya kazi ni vijana kwahiyo ni muhimu jamii ya kimataifa kushirikiana
na serikali na taasisi zingine ili kunusuru kundi hili muhimu kwenye
nchi.
Mkurugenzi
wa TMF nchini, Ernest Sungura akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi
huo wa mafunzo ya bure yanayofadhiliwa na mfuko wake ambapo amesema
kwamba malipo madogo kwa wahariri na waandishi wa habari kunadidimiza
taaluma ya uandishi wa habari pamoja na swala la kutokubobea katika
sekta husika (Specialization).
Wadau
watakaoshiriki kwa ukaribu kwenye mradi huo wakitambulishwa kwa mgeni
rasmi kutoka kushoto ni Dkt. Pilly Said kutoka kitengo cha madawa ya
kulevya hospitali ya Mwananyamala, January Nzisi Mkuu wa Kitengo cha
Mtandao Tume ya Kudhibiti Madawa ya kulevya, Geodfrey Nzowa, Kamishina
Msaidizi wa Jeshi la Polisi, kitengo cha Kupambana na Madawa ya Kulevya,
Bi. Aida Teshe Kaimu Kamishina kutoka Tume ya Kudhibiti Madawa ya
Kulevya (DCC) na Florence Bahati Khambi Afisa Habari kutoka Tume ya
Kudhibiti dawa za kulevya.
FROM THE STATE HOUSE:PRESIDENT JAKAYA KIKWETE MEETS MELINDA GATES AND CANADIAN PRIME MINISTER
President
Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with Mrs. Melinda Gates who is
the Co-Chair and Trustee of the Bill and Melinda Gates Foundation.
NSSF YAENDESHA KAMBI ZA UPIMAJI WA AFYA BURE KANDA YA ZIWA
Lengo la kambi hizi ni kuweza kutoa
elimu na kuwahamasisha wanachama wa NSSF
na wananchi kwa ujumla waweze kujenga tabia
ya kupima afya zao mara kwa mara na kujiwekea mfumo bora wa maisha ili
kuepukana na magonjwa sugu yasiyoambukiza.
Zoezi hili litaanzia mkoa wa Mara,
Manispaa ya Musoma kwenye Viwanja vya
Shule ya Msingi Mkendo, kuanzia tarehe 28/05/2014, kwa siku tatu mfululizo, kuanzia saa mbili
asubuhi mpaka saa kumi na moja Jioni.
Baadae, Kambi hizi zitaendelea katika mikoa ya Shinyanga , Wilaya ya
Kahama, Mkoa wa Geita na Mkoa wa Kagera.
HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA
Huduma mbalimbali zitatolewa bure
kwenye kambi hizi zikiwemo;
Upimaji wa Shinikizo la damu
Upimaji wa sukari kwenye damu-
Kisukari
Upimaji wa hali ya lishe (Uwiano wa Urefu
kwa Unene)
Utoaji wa dawa za Minyoo Ushauri wa kitaalam kwa watakaokutwa
na Matatizo Ushauri nasaha na upimaji hiari wa VVU (UKIMWI) Kutoa vipeperushi vya Maelezo ya
uboreshaji wa Afya.
Huduma zote hizi zitatolewa na NSSF, BURE.
NSSF inaendelea kuwasii na kuwahimiza
wakazi wa kanda ya ziwa kuwa waendelee kujiandikisha kwenye NSSF HIARI Scheme.
NSSF HIARI Scheme ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo, wachimbaji wadogo,
Ushirika wa Bodaboda , Ushirika wa Wakulima pamoja na wanachama wa Mifuko
mingine ya hifadhi ya jamii.
Jiunge na NSSF HIARI Scheme ili uweze
kujipatia mafao bora ya NSSF yakiwemo Bima ya Afya BURE kwa familia nzima
(SHIB), mikopo nafuu ya SACCOS, pamoja
na Mafao bora mengineyo.
Wananchi wa kanda ya ziwa wanakumbushwa
na kuhimizwa kujitokeza kwa wingi ili kupimwa na kupewa ushauri wa afya zao
Bure.
NSSF INAJENGA MAISHA
YAKO YA SASA NA YA BAADAE.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Upimaji Afya Bure Mkoani Mara akifafanua jambo mara baada ya kutembelea banda NSSF ambapo zoezi la upimaji afya lilikuwa likiendeshwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Watu 1080 walipima maambukizi ya virusi vya ukimwi na watu 2020 walipima magonjwa ya kawaida. Kulia ni Meneja wa Mafao ya Matibabu NSSF, Ali Mtulia.
Wakazi wa Mkoa wa Mara wakisubiri kumuona daktari kupata ushauri.
Daktari wa Shirika la Taifa
la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Lucy Simbila (kulia), akimpima shinikizo la damu mmoja
ya watu waliojitokeza kupima
afya mkoani Mara juzi, katika kambi ya Upimaji Afya Bure inayoendeshwa na NSSF
katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Wakazi wa Mkoa wa mara wakiwa kwenye foleni ya kuelekea kwenye vipimo wakati wa zoezi hilo.
Baadhi ya watu waliojitokeza katika zoezi hilo wakiwa kwenye foleni kuelekea kwenye vipimo wakati wa zoezi hilo.
Madaktari wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakimpa ushauri mmoja wa watu waliofika kupima afya.
Madaktari na Maofisa wa NSSF walioendesha kambi ya upimaji wa afya mkoani mara wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment