TANGAZO


Tuesday, June 17, 2014

Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaendelea Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam

Baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwaimbia wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mnazi Mmoja, wimbo wa Afrika Mashariki huku wanafunzi hao wakifuatilia kwa karibu. Wanafunzi hao walitembelea banda la Wizara hiyo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam katika Madhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wakiwaongoza  wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mnazi Mmoja kuimba wimbo wa Shirikisho la Afrika Mashariki wakati walipotembelea banda la wizara hiyo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi ya Umma yanayofanyikakwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Vedastina Justinian akimsikilia mwananchi aliyetembelea banda la wizara hiyo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi ya Umma yanayofanyikakwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Vedastina Justinian akizungumza na televisheni ya Star kwenye banda la wizara hiyo katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO)

No comments:

Post a Comment