TANGAZO


Friday, May 16, 2014

Ziara ya Katibu wa CCM, Abdulrahaman Kinana wilayani Urambo, Tabora

Kinana akikumbatiana na Diwani wa Kata ya Usoke, Kandora Nyanda (CUF), ambaye alikuwepo wakati wa mapokezi wilayani Urambo, Tabora ambako ameanza ziara ya kikazi ya  kuimarisha chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuata Ilani ya CCM mkoani, Tabora leo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia wakati wa mapokezi ya msafara wa Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana katika Kijiji cha Izimbili, wilayani Urambo leo. (Picha zote na Richard Mwaikenda)
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Jimbo la Urambo, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (kushoto),wakisaidia kusakafia katika jengo la maabara ya Shule ya Sekondari ya Uyumbu wakati wa ziara yake wilayani Urambo leo.
Vijana wa Sungusungu wakishangilia wakati wa uzinduzi wa Zahanati ya Izengabotogilwe yenye uwezo wa kuhudumia vijiji vinne, wakati zaiara yake wilayani Urambo leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua shamba la mahindi la Kikundi cha Vijana cha Hiari ya Moyo katika Kijiji cha Ndorobo, wakati wa ziara yake, wilayani Urambo, mkoani Tabora leo. Mahindi hayo yanazalishwa kwa kilimo cha umwagiliaji.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua wodi ya Mama Ngojea katika Hospitali ya Wilaya ya Urambo, mjini Urambo jana,. Jengo hilo limejengwa kwa msaada wa Mbunge wa Jimbo hilo,  Samuel Sitta, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Magreth Sitta, Mfanyabiashara maarufu Mustafa Sabodo na Halmashauri ya wilaya hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Jimbo la Urambo, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (kushoto), wakisaidia ujenzi wa jengo la CCM Tawi la Mabatini mjini Urambo,wakati wa ziara yake ya kuimarisha chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuata Ilani ya CCM mkoani, Tabora leo.

No comments:

Post a Comment