Mwanafunzi Jacson Mnyanyika anayesoma kidato cha tatu katika Shule ya Nzuguni Sekondari, iliyopo Manispaa ya Dodoma, akiwa amevimba jicho kutokana na kipigo toka kwa mwalimu wake wa Taaluma, aliyetambulika kwa jina la Agostino Kagambo.
Mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu cha DCMP kinachomlea Mwanafunzi Jacson Mnyanyika wa kidato cha tatu katika shule ya Nzuguni Sekondari (17) anayedaiwa kupata kipigo kilichomsababishia jeraha ndani ya jicho na Mwalimu wa Taaruma katika shule hiyo. (Picha zote na John Banda)Na John Banda, Dodoma
MWALIMU Agostino Kagambo bado anatumia mfumo wa miaka ya nyuma ya kumpa adhabu ya viboko mwanafunzi jinsi anavyojisikia tena bila kuchagua maeneo ya kuchapa bila kufuata taratibu zilizopo kisheria, hali iliyomfanya kumchapa maeneo mbalimbali ya mwili kiasi cha kumsababishia damu kuvujia jichoni.
Mwalimu Huyo wa Taaruma katika shule ya Sekondari ya Nzuguni manispaa ya Dodoma anatuhumiwa kufanya kitendo hicho Aprl 25 mwaka huu, ambapo anadaiwa kumchapa bila huruma wala kuchagua maeneo ya kuchapa kiasi cha fimbo nyingine kutua kwenye jicho la kushoto na kumsababishia maumivu makali.
Akizungumza kwa masikitiko Mwanafunzi aliyefanyiwa kitendo hicho Jacson Mnyanyika [17] anayesoma kidato cha tatu katika shule hiyo alisema yeye na wenzake watano walipewa adhabu ya viboko 6 kila mmoja na mwalimu huyo kutokana na kudaiwa kushindwa kumaliza kuandika kazi ya vikundi waliyopewa na mwalimu Senyagwa.
Alisema Mwalimu huyo aliamua kutoa adhabu hiyo bila kujali utetezi walioutoa wa kukusanya kazi kwa kiongozi wa kundi lao Kedmon Mzena ambaye kwa wakati huo hakuwepo shuleni hapo, ambapo baada ya wenzake kupata adhabu hiyo yeye akagoma ndipo mwalimu akishirikiana na walimu wengine wakamchangia na Kagambo akamchapa kwa sana kiasi cha fimbo iliyomtulia jichoni alihisi imempasua.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Dodoma Children Maltpupus Centre (DCMP) kinachomlea Mwanafunzi huyo Benaya Alfayo alisema alilipokea kwa masikitiko jambo hilo na kwamba wamempeleka hospital na kuchukuliwa vipimo hivyo wanasubili dkt ajaze fomu ya matibabu toka polisi ili hatua zaidi zifuate.
Naye Mkuu wa Shule hiyo Adamu Mohamed alisema hata yeye alishangazwa na tukio hilo ambapo alimlaumu mwalimu wake huyo ambaye hata hivyo hakuwepo wakati wanafunzi hao walipopewa kazi hiyo na aliporudi kukuta wenzake wakitoa adhabu yeye akaingilia kati, lakini hata hivyo kwakuwa swala hilo lipo polisi hawezi kusema lololte anasubili kitakachaendelea.
‘’Tukio hilo lilitokea katika mazingira ya kutatanisha sana kutokana na wanafunzi hao kufungiwa ndani ya ofisi ya Taaruma ambayo mwalimu Kagambo anaiongoza huku Jackson akiwa katika hali hiyo, na kwa kuwa limefikishwa katika katuo polisi cha Nanenane Nzuguni sina la kusema kwa sasa tusubili majibu ya Dakitari ambaye awali ametuambia Damu imevilia ndani ya jicho la mwanafunzi huyo’’, alisema Mkuu huyo.
No comments:
Post a Comment