Ofisa Mikopo kwa Wateja Wadogo wadogo wa Benki ya KCB Tanzania, Teresia Soko, akitoa mada kuhusiana na baadhi ya huduma za benki hiyo, kwa wafanyabiashara mbalimbali wa mipaka ya Tanzania, ombao walikutana jijini Arusha kujadili mikakati ya kibiashara katika soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Richard Sesibera (kulia), akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Felix Mosha, wakati wa mkutano wa wafanyabiashara mbalimbali kutoka Mikoa ya pembezoni mwa Tanzania. Mkutano huo, uliandaliwa na Benki ya KCB Tanzania na kufanyika jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Felix Mosha akitoa mada wakati wa mkutano ulioandaliwa na Benki ya KCB Tanzania kwa wafanyabiashara wa Mikoa iliyopo mipakani mwa Tanzania, waliokutana jijini Arusha, kujadili maswala mbalimbali ya kibiashara katika soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment