Mwenyekiti wa shirikisho la
kandanda ulimwenguni, FIFA, Sepp Blatter, amesisitiza ilikuwa kosa
kuchagua Quatar kuwa mwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2022.
Katika mahojiano na televisheni nchini Uswizi,
Sepp Blatter aliulizwa iwapo kuiruhusu Quatar kuwa mwenyeji wa kombe
hilo ambalo huchezwa kati ya mwezi Juni na Julai ilikuwa kosa, hasa
ikizingatiwa kuwa hali ya hewa katika nchi hiyo hufikia hadi nyuzijoto
50 wakati huo.Alijibu kwa kukiri na kuongeza kuwa kila mtu hukosea maishani. Alipinga madai kwamba taifa hilo lilikuwa limelipia michezo hiyo.
Aliongeza kuwa kamati inayojumuisha maafisa wa FIFA walikuwa wamedhibitisha uwezekano wa taifa hilo kuwa mwenyeji ijapokuwa walikuwa wamepokea taarifa kuhusu vipimo vya juu vya joto.
Alisema kwamba michezo hiyo badala yake inaweza kusogezwa hadi miezi ya mwisho wa mwaka, wakati vipimo vya joto vitakuwa vimepungua.
No comments:
Post a Comment