Ripoti mpya iliyotayarishwa na
wachunguzi wa umoja wa mataifa kuhusu visa vya ukiukaji wa haki za
binadamu inasema haki za binadamu nchini Ukraine zimezorota kwa kiwango
kikubwa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, maandamano ya amani
kwa wakati mwingi yanageuka na kuwa vurugu, waandishi wa habari pamoja
na wachunguzi wa kimataifa wanakamatwa na kuzuiliwa huku wapinzani
wakiuwawa.Ripoti hiyo inasema ukiukaji wa sheria umekithiri maeneo ya Mashariki na Kusini na kumekuwa na visa vya watu kulengwa katika njama za mauaji, kuteswa na kutekwa nyara.
Uhalifu huu unatekelezwa na vikosi vinavyoipinga serikali mashariuki mwa Ukraine. Urusi inasema kuwa ripoti hiyo inaegemea upande mmoja na imejaa mapungufu makubwa.
No comments:
Post a Comment