TANGAZO


Thursday, May 15, 2014

Wakulima wamhuzunisha Kinana kwa kumtolea kilio cha kudhulumiwa malipo ya tumbaku Sikonge


Katibu Mkuu wa CCM, akiwa na huzuni alipokuwa akisikiliza kilio cha wakulima kudhulumiwa asilimia 64 za malipo yao ya mauzo ya tumbaku na vya vya ushirika katika Kata ya Kitunda, wilayani Sikonge, mkoani Tabora. Pia wakulima hao walisema kuwa wanadai zaidi ya sh. bilioni 112 za mauzo hewa ya  pembembejeo.
 Mkulima wa zao la tumbaku katika Kata ya Kitunda, wilayani Sikonge, akielezea mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana jinsi viongozi wa vyama vya ushirika wanavyosaini mkataba hewa wa pembejeo zenye thamani ya s dola za kimarekani 150.
 Mwakilishi wa wakulima wa tumbaku katika Chama cha Ushirika  cha Tumbaku Mkoa wa Tabora, Rameck WETCO, Rameck Mnyama, akielezea  jinsi viongozi wa ushirika huo wanavyowanyonya wakulima wa zao hilo, wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kitunda uliohutubiwa na KKatibu Mkuu wa CCM, Nduigu Kinana. Ambapo hadi sasa wanaudai ushirika dola za kimarekani 76.
 Katibu Mkuu akisalimiana na waalimu pamoja na wananchi alipowasili kukagua n ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari Kiwele, iliyopo Kata ya Kitunda, wilayani Sikonge.
 Kinana akikagua maabara katika shule hiyo ya kata.
 Kinana akikagua ndani ya maabara hiyo ambayo ujenzi wake utakamilika hivi karibuni.
 Kaimu Mhandisi wa Ujenzi Wilaya ya Sikonge, Eng. Butele Jilala akielezea kuhusu ujenzi wa  maabara hiyo ya kufundishia masomo ya Fizikia, Baioloji na kemia.
 Mganga Mfgawidhi wa Kituo cha Afya cha Kitunda, wilayani Sikonge, Dk Sylivanus Kabatula akitoa maelezo wa Ndugu Kinana kuhusu ucheleweshwaji wa ujenzi wa jengo la upasuaji unaofanywa na mkandarasi Humprey katika kituo hicho cha afya, hivyo kuwakosesha wananchi huduma za matibabu.
 Kinana akikagua jengo la upasuaji la Kituo cha Afya cha Kitunda, wilayani Sikonge.
 Wasanii wa kabila la wasukuma wakitumbuiza kwa ngoma ya zeze wakati Ndugu Kinana alipowasili kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Kitunda.
 Mbunge wa Jimbo la Sikonge, Said Nkumba akielezea kwa masikitiko jinsi wakulima wa zao la tumbaku wanavyodhulimiwa mabilioni na viongozi wa vyama vya ushirika wilayani Sikonge na Mkoa wa Tabora.
"Kazi yetu CCM ni kuendelea  kuisimamia Serikali ili wananchi wapate haki zao, kwani walioomba kura kwenu ni CCM, hivyo tukikaa kimya  tutalaumiwa , najua kwa ziara hii hapa Kitunda itafanya mambo yabadilike, hiyo ndiyo salmu yetu kwenu, asanteni" amesema Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipokuwa anahutubia katika Kata ya Kitunda, Sikonge leo. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Katibu Mkuu  wa CCM, Ndugu Kinana akihutubia katika mkutano huo na kukemea kitendo cha vyama vya ushirika kuwadhulumu bila huruma wakulima wa tumbaku. Pia alisikitishwa na kitendo cha serikali akiwemo waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika kutwatembelea wakulima kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi. Pia alisema kama kiongozi umeshindwa kuwatumikia w2ananchi ni bora uachie ngazi.
 Sehemu ya umati wa watu waliokuwepo kwenye mkutano huo.
 Ndugu Kinana akisoma vijiji vitavyopata umeme wilayani Sikonge mwaka huu wa fedha.

No comments:

Post a Comment