Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akionesha jedwali la alama za ufuatiliaji wa utendaji wa huduma za afya ya mzazi na mtoto wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Kuongeza kasi ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto katika ukumbi wa mikutani wa kimataifa wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni Naibu Waziri wa Afya Dkt Kebwe Sthephen Kebwe.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi kitabu Bibi Halima Shariff, mmoja wa wadau wa afya kutoka katika kundi la marafiki wa maendeleo. pamoja na kitabu hicho pia kuna jedwali (score-card) la alama za ufuatiliaji wa utendaji wa huduma za afya ya mzazi na mtoto wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Kuongeza kasi ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto katika ukumbi wa mikutani wa kimataifa wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni naibu Waziri wa Afya Dkt Kebwe Sthephen Kebwe.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete na wagemi wengine wakifuatilia maelezo wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Kuongeza kasi ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto katika ukumbi wa mikutani wa kimataifa wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni naibu Waziri wa Afya Dkt Kebwe Sthephen Kebwe.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Kuongeza kasi ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto katika ukumbi wa mikutani wa kimataifa wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Kuongeza kasi ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto katika ukumbi wa mikutani wa kimataifa wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Na
Magreth Kinabo – Maelezo
15/05/2014
RAIS
Jakaya Kikwete amewataka
Wakuu wa mikoa na wilaya
kuhakikisha kuwa wanasimamia Mpango Mkakati ulioboreshwa
wa Kuongeza Kasi ya Kupunguza
vifo vya Uzazi vya wakinamama na watoto hususan wachanga ili kutimiza malengo ya millennia
namba nne na tano ifikapo mwaka 2015.
Aidha Rais Kikwete aliagiza viongozi wa mapango wa
Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kuliingiza suala la afya katika mpango huo.
Changamoto hiyo imetolewa leo na Rais Kikwete kabla ya kuzindua mpango huo, ulioenda sambamba na uzinduzi wa kadi
ya ufuatiliaji(scorecard) ambayo itakuwa
inaonesha tathimini na ya maendeleo na mkakati huo kwa kila mkoa na wilaya.
Rais Kikwete aliwataka wakuu hao na watendaji wao
kutoa ripoti ya kadi ya ufuatiliaji kila baada ya miezi minne. Kadi hiyo, ambayo
itakuwa na taarifa ya maendeleao ya kupunguza vifo vya watoto wachanga, chini
ya miaka mitano na wakinawajawazito.
Uzinduzi huo, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano
wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares Salaam.
Alisema vifo
vya uzazi vya wakina mama vimepungua kutoka 578 kwa vizazi hai 100,000 mwaka
2005 na kufikia vifo 454 kwa vizazi hai 100,000 kwa sasa, wakati lengo la milenia
ni vifo 193 kwa vizazi hai 100,000.
“Bado tuna
safari ndefu ninawataka wakuu wa mikoa na wilaya kuchulikia jambo hili kwa
umakini na kulipa kipaumbele kwani
jukumu hili si la waganga wakuu wa mikoa au wilaya na mimi nitakuwa
ninafuatilia kwa kuwa jambo hili, lipo mikononi
mwangu. Ninataka kulifuatialia kabla
sijamaliza kipindi cha uongozi wangu,” alisema Rais Kikwete.
Aliongeza kuwa vifo hivyo vya wakina mama na watoto
hutokea lakini havifatiliwi ndio maana inakuwa vigumu kubaini njia za
kuvipunguza.
"Baya zaidi wanakufa kwa sababu zinazoweza kuzuilika, kadi ya ufuatiliaji ikifuatiliwa na wakuu wa mikoa itasaidia kupunguza vifo,” alisisitiza.
"Baya zaidi wanakufa kwa sababu zinazoweza kuzuilika, kadi ya ufuatiliaji ikifuatiliwa na wakuu wa mikoa itasaidia kupunguza vifo,” alisisitiza.
Alisema ikiwa
watoto waliochini ya miaka mitano na wakinamama wajawazito watazingatia masuala
ya lishe bora kwa kipindi cha siku 1000 pia itasaidia kupunguza vifo hivyo.Huku
akisema vyakula hivyo vipo majumbani kinachohitajika ni elimu.
Aliwataka wakimama
kuzingatia uzazi wa mpango(nyota ya kijani ) ili kusaidia kupunguza tatizo
hilo, pia kushirikisha wanaume juu ya jambo hilo.
Rais Kikwete pia alisema asilimia 51 ya wakina
wanaojifungua huhudumiwa na watalaamu wenye ujuzi, wakati malengo ya milinea ni
asilimia 80, hivyo bado kuna changamoto
ya asilimia 29.
Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt.
Kebwe Stephen Kebwe, alisema kwa
kipindi cha mwaka huu wanampango wa kuajiri watalaamu hao 11,021.
Alisema
Tanzania imefanikiwa kutimiza lengo la milinea namba nne kabla ya wakati kwa
kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano kwa kiwango cha 54 kwa watoto wanaozaliwa
1000, kutoka 165 kwa wataoto wanaozaliwa 1000 mwaka 1990. Alizitaja nchi
nyingine zilizofanikiwa ni Rwanda,
Malawi,Ethiopia Rwanda na Malawi.
Naye mwakilishi wa wakuu hao, Dk.
Christine Ishengoma alisema uwajibikaji
wa viongozi na watendaji ni jambo la
muhimu katika kutekeleza mpango huo, hivyo suala hilo linawezekana.
Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya
Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dk. Deo Mutasiwa alisema sheria ndogondogo zinatengenezwa ili
kuwezesha mpango huo kufikia lengo.
Dk. Mutasiwa alizitaka halimashauri kutumia
vyanzo vyake vya mapato ya ndani kwa asilimia 60 kuwekeza katika masuala ya
afya, elimu maji na barabara za vijijini.
Alisema hivi sasa wako katika mchakato wa
kupata kibali cha kuwaezesha watoa huduma wa afya wanaomba nafasi za kazi
kufanyia kazi maeneo wanayotoka.
No comments:
Post a Comment