*Awaonya wanaojipitisha
Katibu wa ofisi ya mbunge wa jimbo la Kalenga Bw. Martin Simangwa kushoto akikabidhi msaada wa bati 80 kwa mwenyekiti wa kijiji cha Mlanda Bw Vitaris Samila huku wajumbe wa serikali ya kijiji wakishuhudia.
|
viongozi wa serikali ya kijiji cha Wangama wakimsikiliza katibu wa mbunge wa jimbo la Kalenga alipofika kukabidhi msaada wa bati 100 na saruji mifuko 50.
|
Bw. Simangwa akizungumza na viongozi wa kijiji cha wangama.
|
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kalenga Bw Simangwa kulia akikabidhi msaada wa bati kijiji cha Negabihi jana. |
Na Francis Godwin Blog
MBUNGE wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa Godfrey Mgimwa amekabidhi msaada wa bati 280 na saruji mifuko 50 kwa katika kata ya Wangama na Mlanda ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi alizozitoa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Dr Wiliam Mgimwa huku akiwataka wananchi kuwapuuza watu wanaojipitisha kutaka ubunge mwaka 2015.
Akikabidhi msaada huo wenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 6.7 jana katibu wa mbunge Mgimwa Martine Simangwa alisema kuwa mbunge Godfrey Mgimwa ameanza kutekeleza ahadi mbali mbali ambazo aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Marehem Dr Mgimwa alipata kuzitoa katika maeneo mbali mbali ya jimbo hilo.
“Mheshimiwa Godfrey Mgimwa mbunge wetu wa jimbo la Kalenga ameanza kutimiza ahadi zilizotolewa na marehemu Dr Mgimwa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi mbali mbali zilizotolewa na mbunge huyo … hadi sasa ahadi mbali mbali zimeendelea kutekelezwa na Godfrey Mgimwa kama alivyopata kuwaahidi wananchi wakati wa kampeni”alisema Simangwa .
Kuwa msaada huo wa bati 100 na saruji mifuko 50 ambao umetolewa katika kijiji cha Wangama kwa ajili yha ukarabati wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Wangama wakati kijiji cha Negabihi zimetolewa bati 100 na bati 80 zimetolewa kijiji cha Mlanda na kuwa zoezi la kukamilisha ahadi mbali mbali za marehem Dr Mgimwa zinaendelea kutekelezwa katika maeneo yote .
Alisema kuwa hadi mwakani sehemu kubwa ya ahadi hizo itakuwa imetekelezwa na mbunge Godfrey Mgimwa na kuwataka wananchi wa jimbo la Kalenga kwa sasa kupuuza wanasiasa wa vyama vya upinzani na wale wa CCM ambao wameendelea kuzunguka jimboni kwa ajili ya kuwadanganya wananchi kwa ajili ya mwaka 2014
Simangwa alisema kuwa wapo baadhi ya watu wasiomtakia mafanikio mbunge Godfrey Mgimwa walipata kuzusha kuwa mbunge huyo amekamatwa uwanja wa Ndege Dar es Salaam akitaka kukimbilia Uingereza kuishi jambo ambalo si kweli na wapo ambao walieneza kuwa mbunge huyo amegoma kuapishwa kwa madai kuwa hataka kuliongoza jimbo hilo.
” Watu hao hao wamekuwa wakieneza uongo kwa wananchi dhidi ya mbunge Godfrey Mgimwa ila ukweli ni huu mbunge wenu anawapenda sana na hadi sasa yupo bungeni Dodoma akiendelea na vikao vya bunge la bajeti na mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho atafanya ziara hivyo wapuuzeni wote wanaoeneza uongo huo”
Bila kuwataja majina watu hao na vyama vyao alisema kuwa tayari wameanza kukasilishwa na utekelezaji mzuri wa ahadi mbali mbali unaofanywa na mbunge Godfrey Mgimwa.
Katibu huyo alisema kwa sasa Mgimwa ni mbunge wa jimbo hilo wa wananchi wote bila kujali itikadi za vyama wala dini zao na kuwa moja kati ya malengo yake ni kugombea tena ubunge mwaka 2015 hivyo kwa kipindi hiki kifupi cha mwaka mmoja uliobaki ni kuona ahadi zote zilizotolewa na mbunge aliyefariki zinatekelezwa na kusaidia mambo mengine ya ziada pale yanapojitokeza.
Akishukuru kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Kalenga mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Negabihi Gaudence chung’unge alisema kuwa wao kama wananchi wataendelea kumuunga mkono mbunge huyo na kuwa hawapo tayari kuwasikiliza wale wanaojipitisha kwa wakati huo.
No comments:
Post a Comment