Vyama vya wafanyakazi nchini
Uturuki vimeitisha mgomo wa siku moja kulalamika dhidi ya Serikali
kufuatia ajali mbaya zaidi ya mgodini kuwahi kutokea nchini humo.
Viongozi wa vyama vya wafanyakazi wanalalamika
kuwa kuuzwa kwa migodi ya umma kwa watu binafsi kumechangia pakubwa
katika kudorora kwa hali ya usalama katika viwanda.Makundi ya waokozi yangali yanajaribu kuwafikia zaidi ya wafanyakazi wengine 100 ingawa juhudi zao zingali zinavurugwa na mioto inayowaka kwenye maeneo ya mgodi huo.
Waokoaji wenyewe imelazimu watibiwe kwa uchovu na kupumua moshi.
Mwandishi wa BBC katika Soma anasema kuwa baadhi familia za waliofariki wamekasirishwa na hatua ambazo zimechukuliwa na Serikali kufikia sasa.
Jumanne polisi walipambana na waandamanaji katika miji ya Ankara na Istanbul na Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan alizomwa alipotembelea eneo la ajali hiyo ya mgodi.
No comments:
Post a Comment