* Wakusanya zaidi ya sh. bilioni 115 hadi kufikia Machi 2014
Meneja wa
Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Kanda ya
Mashariki Bw. Sayi Lulyalya akiwaeleza waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam (hawapo pichani),
kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na mfuko huo, ikiwemo kukusanya zaidi ya bilioni 115 hadi kufikia
machi 2014 sawa na asilimia 94 ya lengo. Kushoto ni Kaimu Meneja Masoko wa
Mfuko huo, Bi. Rehema Mkamba. (Picha na Jojina Misama)
Frank
Mvungi-Maelezo
MFUKO wa
pensheni wa LAPF umefanikiwa kusajili wanachama 20,214 kufikia mwezi machi 2014
wakati lengo lilikuwa wanachama 15,287 katika kipindi hicho.
Hayo yamesemwa
na Meneja wa Kanda ya Mashariki wa mfuko huo bw. Sayi Lulyalya wakati wa
mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Lulyalya alisema
ongezeko hilo ni matokeo ya kuwepo kwa utekelezaji wa sera nzuri zenye kuwajali
wanachama wa mfuko huo na jaamii kwa ujumla.
Alisema kuwa
mfuko huo umepanga kuongeza wanachama wake hadi kufikia 122,595 kwa kuwa
mwitikio wa wananchi kujiunga na mfuko huo umekuwa chanya kwa kiasi kikubwa.
“Tumekuwa na
wanachama kutoka sekta binafsi ambao nao wameonyesha mwamko wa kujiunga na
uchangiaji wa hiari katika mfuko wetu ikiwa ni sehemu ya kujiwekea akiba “
alisema Lyalya.
Katika kutoa
elimu kwa umma kuhusu faida wanazopata wanachama wa mfuko huo Lyalya alisema
wamekuwa wakitoa elimu kwa njia ya redio,Televisheni,Magazeti na na Makongamano.
Naye Kaimu Meneja Masoko wa Mfuko huo Bi Rehema Mkamba
alisema kuwa Mfuko huo umekuwa ukichangia katika huduma za kijamii ambapo
katika mwaka wa fedha 2013/2014 shilingi milioni 200 zilitengwa kwa ajili ya shughuli za
kijamii katika sekta za afya,elimu na kusaidia watu wenye mahitaji maalum.
Katika makusanyo
mfuko ulijiwekea malengo ya kukusanya shilingi bilioni 122.7 ambazo ni michango
ya wanachama na malimbikizo,ambapo hadi kufikia mwezi machi 2014 mfuko umeweza
kukusanya bilioni 155.5 sawa na
asilimia 94 ya lengo kwa kipindi
hicho.
No comments:
Post a Comment