TANGAZO


Thursday, May 15, 2014

Mwenyekiti wa TPSF, Reginald Mengi, afungua maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Uturuki na Nigeria nchini Tanzania

Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi (kushoto), Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu (katikati) na Balozi Mdogo wa Nigeria, Adamu Mussa wakiwa wamesimama kuomboleza ajali ya mgodi wa mkaa wa mawe, iliyotokea leo nchini Uturuki, kabla ya kuzindua maonesho ya siku tatu ya Kimataifa ya Biashara ya Uturuki na Nigeria nchini Tanzania, ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu, akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonesho ya siku tatu ya Kimataifa ya Biashara ya Uturuki na Nigeria nchini Tanzania, Dar es Salaam leo.
Mshereheshaji wa hafla hiyo, Pascal Mayalla akifafanua jambo wakati wa kuomboleza ajali ya mgodi wa makaa ya mawe wa Uturuki wakati wa uzinduzi wa maonesho ya siku tatu ya Kimataifa ya Biashara ya Uturuki na Nigeria nchini Tanzania, Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Maonesho ya Biashara ya Atlantic ya Nigeria, Ayodeji Olugbade, akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonesho hayo. Kushoto ni mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi.
Mkurugenzi wa Mauzo wa Kimataifa wa Kampuni ya Meridyen ya Uturuki, Nuvit Becan, akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonesho ya siku tatu ya Kimataifa ya Biashara ya Uturuki na Nigeria nchini Tanzania, Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA), Dk. Adelhelm Meru, akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonesho ya siku tatu ya Kimataifa ya Biashara ya Uturuki na Nigeria nchini Tanzania, Dar es Salaam leo. Kushoto ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi.
Balozi Mdogo wa Nigeria, Adamu Mussa, akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonesho ya siku tatu ya Kimataifa ya Biashara ya Uturuki na Nigeria nchini Tanzania, Dar es Salaam leo.
Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi (wa pili kushoto), kuzungumza na kisha kuyazindua rasmi maonesho hayo.
Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi, akizungumza wakati alipokuwa akizindua maonesho ya siku tatu ya Kimataifa ya Biashara ya Uturuki na Nigeria nchini Tanzania, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu na katikati ni Balozi Mdogo wa Nigeria, Adamu Mussa.
Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi, akizungumza wakati alipokuwa akizindua maonesho ya siku tatu ya Kimataifa ya Biashara ya Uturuki na Nigeria nchini Tanzania, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu na katikati ni Balozi Mdogo wa Nigeria, Adamu Mussa.
Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi, akifafanua jambo, wakati alipokuwa akizungumza wakati akizindua maonesho ya siku tatu ya Kimataifa ya Biashara ya Uturuki na Nigeria nchini Tanzania, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu na katikati ni Balozi Mdogo wa Nigeria, Adamu Mussa.
Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi, akieleza jambo, wakati alipokuwa akizungumza wakati akizindua maonesho ya siku tatu ya Kimataifa ya Biashara ya Uturuki na Nigeria nchini Tanzania, jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa katika uzinduzi wa  maonesho ya siku tatu ya Kimataifa ya Biashara ya Uturuki na Nigeria nchini Tanzania, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya washiriki wa maonesho hayo, wakiwa katika hafla ya uzinduzi huo jijini leo.
Baadhi ya washiriki wa maonesho hayo, wakimsikiliza mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi, jijini leo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi (kushoto), akiwa na Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu.
Viongozi katika meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi (katikati), wakati wa uzinduzi huo, jijini leo. Kushoto kwake ni Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu.
Viongozi katika meza kuu wakibadilishana mawazo, wakati wa uzinduzi huo, jijini leo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi (katikati), akikata utepe kuzindua maonesho ya siku tatu ya Kimataifa ya Biashara ya Uturuki na Nigeria nchini Tanzania, Dar es Salaam leo. Kulia ni Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA), Dk. Adelhelm Meru.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi (katikati), akipatiwa maelezo na mmoja wa washiriki wa maonesho hayo (kushoto), wakati alipokuwa akitembelea mabanda kwenye maonesho hayo, mara baada ya kuyazindua jijini leo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi (katikati), akipatiwa maelezo na mmoja wa washiriki wa maonesho hayo (kushoto), wakati alipokuwa akitembelea mabanda kwenye maonesho hayo, mara baada ya kuyazindua jijini leo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi (kushoto), akipatiwa maelezo na mmoja wa washiriki wa maonesho hayo, Mohannad Aldolati (kulia), Meneja Mauzo wa Kanda wa Kampuni ya Fira Color ya Uturuki.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi (kushoto), akizungumza jambo na mmoja wa wananchi kwenye maonesho hao.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi (katikati), akipewa zawadi ya kapeti na mmoja wa washiriki wa maonesho hayo (kushoto kwake), Mkurugenzi wa Kampuni ya mirac, Mesut Karademir.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi (katikati), akipewa zawadi ya kapeti na mmoja wa washiriki wa maonesho hayo (kushoto kwake), Mkurugenzi wa Kampuni ya mirac, Mesut Karademir.

Nyendo Mohamed

MWENYEKITI Mtendaji wa Kampuni za IPP, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Reginald Mengi amesema kuwa njia pekee ya kukua kwa haraka uchumi wa Tanzania ni kuruhusu wawekezaji kutoka nje.

Pia amesema anashangazwa sana na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakipinga kuwepo kwa wawekezaji nchini.

Aliyazungumza hayo leo, mbele ya wanahabari, wakati akifungua maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Uturuki na Nigeria, yatakayofanyika kwa siku tatu nchini.

Mengi alisema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na nchi ya Uturuki umekuwa mzuri na ndio maana wamekuwa wakishirikiana katika masuala mbalimbali ya kibiashara ili kukuza uchumi.

Alibainisha Uturuki wamekuwa wazalishaji wazuri wa biadhaabora na bei yao ni rafiki hivyo watu watembelee maonesho hayo kujionea bidhaa hizo

''Watanzania wanatakiwa kuamini kuwa uwekezaji unasaidia nchi kukuza uchumi katika nchi yoyote hata mataifa tajiri yamekuza uchumi kwa njia hiyo''alisema

Hata hivyo Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Ali Davutoglu alisema kuwa Tanzania ni nchi muhimu barani Afrika katika biashara.

Davutoglu alisema maonesho hayo ni kwaajili ya kuoanua wigo wa biashara si tu kwa Tanzania bali katika bara zima la Afrika.

Alisisitiza kuwa wataendelea kudumisha ushirikiano huo na kuhakikisha kuwa kila mmoja anafaidiaka kiuchumi.
 

No comments:

Post a Comment