Wanawake nchini Iran wameanza
kuweka picha zao katika akaunti maalum ya Facebook wakiwa bila hijab au
wakiwa hawajajifunika vichwa vyao.
Ukurasa huo wa facebook unaitwa “uhuru wangu''Hadi sasa, ukurasa huo una takriban picha 150.
Picha hizo zinawaonyesha wanawake wakiwa kwenye fuo za bahari, katika barabara, mashambani, wakiwa peke yao, wakiwa na marafiki, na wengine wakiwa na wapenzi wao- lakini la muhimu, wote bila hijabu vichwani.
Nyingi kati ya picha hizo zimeandikwa maneno machache kama vile, “sijihisi kuvalia hijab, mimi pia napenda miale ya jua na upepo katika nywele yangu. Je, hiyo ni dhambi kubwa?”
Masih Alinejab, mwanahabari anayehusika na maswala ya kisiasa, ambaye ndiye mwanzilishi wa ukurasa huo na ambaye ni raiya wa Iran anayeishi Uingereza anasema kuwa nywele yake ilikuwa imemfanya kuwa kama mateka kwa serikali.
Anaongezea kuwa serikali bado ina mateka wengi wa aina hiyo.
Alinejab alipata wazo hilo baada ya kuweka picha zake kwenye ukurasa wake binafsi wa facebook akiwa bila hijab.
Picha hizo zilipendwa na maelfu ya watu, na hivyo wanawake wengine wakaanza kutuma picha zao, jambo lililomfanya kuanzisha ukurasa huo.
"Tatizo langu sio kuvalia vitambaa kichwani. Tatizo langu sio kukosa la kufanya,” aliandika mwanamke mmoja kwenye ukurasa huo wa facebook. "Uhuru wa kujificha unamaanisha nitakuwa ninavyopendekeza kuwa, angaa kwa sekunde chache,” aliandika mwingine.
Swala la hijab lina tetesi nchini Iran.
Kampeni ya mabango iliyofanywa majuzi ili kuwakumbusha wanawake kujifunika, ilikejeliwa kwa kuwafananisha wanawake na chokleti iliyofungwa kenye pakiti.
Hata hivyo, wengi wanapendekeza kuvalia hijab na kusema kuwa ni sheria muhimu ya kiislamu. Kulikuwepo na maandamano Tehran juma lililopita, waandamanaji wakisisitiza sheria hizo kutiliwa mkazo zaidi.
No comments:
Post a Comment