Serikali ya Mali imepuuza mzozo
unaotokota kati yake na shirika la fedha duniani IMF kuhusu hatua ya
kumnunulia Rais wa nchi hiyo ndege ndege kuu kuu kwa kima cha dola
milioni arubaini, hata baada ya kuahidi kulipatia swala la umasikini
kipaombele.
Maafisa wa Mali watahojiwa hii leo katika mkutano wa wafadhili hao wa kimataifa.Shirika la fedha Duniani I-M-F ndilo lilihoji kwa ununua wa ndege hiyo ulifanyika wakati nchio hiyo ina mambo megi muhimu ya kushughulikia kuliko kumnunulia Rais ndege iliyozeeka.
Mwakilishi wa IMF nchini Mali, (Anton Op de Beke) aliambia BBC kuwa hawajaelezewa kikamilifu kwa nini serikali ilifanya hivyo.
Lakini waziri wa mawasiliano wa nchi hiyo Rais wa nchi hiyo ,Mamadou Camara, alisema kuwa walikuwa wameieleza serikali kuhusu mpango wa kununua ndege hiyo na kuwa shirika hilo lina uhusiano mzuri tu na shirika la IMF.
Wahisani wa kimataifa, ambao wako nchini Mali, wanatarajiwa kuhoji ununuzi huo pamoja na kandarasi ya ulinzi itakayogharimu serikali hiyo dola milioni miambili.
Mwaka mmoja uliopita , wahisani waliahidi kuipa Mali dola bilioni nne kuisaidia serikali kukarabati nchi baada ya vita.
No comments:
Post a Comment