TANGAZO


Friday, May 9, 2014

Uzinduzi wa Shindano la Blue Band la kujishindia Mradi wa sh. mil 19 kwa Shule za Msingi

Mwakilishi Mkazi wa Kampuni ya Unilever, watengenezaji wa bidhaa mbalimbali za matumizi ya nyumbani, Raymond Banda, akizungumza wakati wa uzinduzi wa shindano la Blue Band kwa shule za msingi, Dar es Salaam jana, ambapo shule itajishindia mradi wa thamani ya sh. milioni 19, wanafunzi kushinda safari za kwenda Marekani pia walimu kujishindia fedha taslimu sh. laki 5 mpaka milioni moja. Wapili kulia ni mgeni rasmi katika hafla hiyo, Kaimu Kamishana wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  (Veta), Dk. Leticia Say. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mgeni rasmi, Kaimu Kamishana wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  (Veta), Dk. Leticia Say, akizungumza wakati alipokuwa akizindua shindano la Blue Band kwa shule za msingi, Dar es Salaam jana, ambapo shule itajishindia mradi wa thamani ya sh. milioni 19, wanafunzi kushinda safari za kwenda Marekani pia walimu kujishindia fedha taslimu sh. laki 5 mpaka milioni moja. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Kampuni ya Unilever, watengenezaji wa bidhaa mbalimbali za matumizi ya nyumbani, Raymond Banda.
Kaimu Kamishana wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  (Veta), Dk. Leticia Say (wa tatu kulia), Mwakilishi Mkazi wa Kampuni ya Unilever, watengenezaji wa bidhaa mbalimbali za matumizi ya nyumbani, Raymond Banda (kushoto) na Ofisa Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe, Bupe Ntoga (wa pili kulia), wakifurahi kwa kupiga makofi na wanafunzi wa Shule za Msingi za Diamond na Bunge, wakati alipozindua shindano la Blue Band kwa shule za msingi, ambapo shule itajishindia mradi wa thamani ya sh. milioni 19, wanafunzi kushinda safari za kwenda Marekani pia walimu kujishindia fedha taslimu sh. laki 5 mpaka milioni moja.
Kaimu Kamishana wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  (Veta), Dk. Leticia Say (kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Kampuni ya Unilever, watengenezaji wa bidhaa mbalimbali za matumizi ya nyumbani, Raymond Banda (kulia) na Ofisa Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe, Bupe Ntoga (katikati), wakifurahi na wanafunzi wa Shule za Msingi za Diamond na Bunge, wakati alipozindua shindano la Blue Band kwa shule za msingi, ambapo shule itajishindia mradi wa thamani ya sh. milioni 19, wanafunzi kushinda safari za kwenda Marekani pia walimu kujishindia fedha taslimu sh. laki 5 mpaka milioni moja. 
Kaimu Kamishana wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  (Veta), Dk. Leticia Say (katikati), akioneshwa jadweli la shindano kwa wanafunzi na Shule na Mwakilishi Mkazi wa Kampuni ya Unilever, watengenezaji wa bidhaa mbalimbali za matumizi ya nyumbani, Raymond Banda, mara baada ya kuzindua shindano hilo la Blue Band kwa Shule za Msingi, Dar es Salaam jana.
Wanafunzi wa Shule za Msingi za Diamond na Bunge wakicheza muziki wa Kwaito, wakati wa uzinduzi wa shindano la Blue Band kwa shule za msingi, ambapo shule itajishindia mradi wa thamani ya sh. milioni 19, wanafunzi kushinda safari za kwenda Marekani pia walimu kujishindia fedha taslimu sh. laki 5 mpaka milioni moja.
Mwakilishi wa Kampuni ya Unilever, akielezea jinsi ya namna ya kubandika stika za shindano hilo.
Mmoja wa wanafunzi wa Shule za Msingi za Diamond na Bunge, waliokuwepo kwenye uzinduzi huo, akionesha namna ya kubandika stika za shindano hilo la Blue Band.
Mmoja wa wanafunzi wa Shule za Msingi za Diamond na Bunge, waliokuwepo kwenye uzinduzi huo, akionesha namna ya kubandika stika za shindano hilo la Blue Band. 
Moja ya Bidhaa za Kampuni ya Unilever, Blue Band Margarine, zikiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa shindano hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Unilever, wakiwa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika hafla ya uzinduzi huo.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi za Diamond na Bunge wakiwa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi za Diamond na Bunge, wakiwa katika uzinduzi huo.
Ofisa Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe, Bupe Ntoga, akikabidhiwa zawadi ya bidhaa ya Blue Band na Mwakilishi Mkazi wa Kampuni ya Unilever, watengenezaji wa bidhaa mbalimbali za matumizi ya nyumbani, Raymond Banda. Kulia ni Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Kaimu Kamishana wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  (Veta), Dk. Leticia Say, ambaye naye alikabidhiwa yake.
Mmoja wa wanafunzi wa Shule za Msingi za Diamond na Bunge, walishiriki katika uzinduzi wa shindano hilo, akisoma bango lililokuwa likielezea kuhusu shindano na zawadi kwa shindano hilo.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi za Diamond na Bunge wakijipatia chakula wakati wa uzinduzi huo.
Mgeni rasmi, Kaimu Kamishana wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  (Veta), Dk. Leticia Say, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, mara baada kulizindua shindano hilo, la Blue Band kwa shule za Msingi.

No comments:

Post a Comment