WALIMU
Wakuu wa Shule ya Sekondari Chikola na msingi ya Chidete zilizofanya
vibaya kwenye matokeo ya ufaulu Kiwilaya zimeshindwa kujitokeza
hadharani kwa Mkuu wa Wilaya ya Bahi Betty Mkwasa kuchukuwa zawadi zao.
Tukio
hilo ambalo mwandishi wa habari hii alishuhudia lilitokea hivi
karibuni kwenye maadhimisho ya wiki ya elimu,baada ya Mkuu wa Wilaya
kuwataka wachukuwe zawadi zao ikiwemo sanamu ya mpingo na kikombe
kidogo hali ambayo wadau na wanafunzi walilazimika kuwazomea na kubezwa.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Wilaya hiyo alisema walimu hao walitakiwa kupokea
zawadi hizo kama changamoto kwao kwa kufanya vibaya kwenye ufaulu wa
wamafunzi katika shule hizo ikiwemo hiyo ya sekondari na msingi.
“Shule
ya sekondari ya Chikola imekabidhiwa zawadi ya sanamu ya kinyango cha
mpingo,kutokana na kushindwa kufaulisha mwanafunzi hata mmoja kwa miaka
mingi toka ianzishwe shule hiyo,hii ni pamoja na shule ya msingi ya
Chidete ambayo imepewa zawadi ya kombe dogo haijafaulisha mwanafunzi wa
kiingia kidato cha kwanza”Alisema..
Betty
akizungumza na halaiki wa wananchi na wadau wa elimu alisema kuwa
pamoja na walimu hao kugoma kujitokeza kuchukua zawadi hizo atahakikisha
anazipeka yeye mwenyewe ili akadhikabidhi kwa walimu hao mbele ya
wanafunzi wao.
Alisema
zawadi hizo zimetolewa ili kutoa changamoto kwa shule zingine kuongeza
kasi ya maendeleo ya elimu ikiwa na ufaulu na hatimaye kuondokana na
nafasi hiyo ya mwisho kitaaluma katika wilaya ya Bahi.
Hata
hivyo amewataka wazazi na wadau wa elimu wa wilaya hiyo kujenga
mahusiano mazuri katika mazingira ya miundombinu inayohitajika kwa
walimu na wanafunzi ambao shule zao zimekuwa zifanya vibaya katika
matokea ya ufaulu wa wanafunzi.
Alisema
pamoja na changamoto zilizopo kwenye shule pia zinachangiwa na wazazi
na wadau wa elimu ya kutopenda kuchangia michango mbalimbali ambayo
inayoweza kuboresha elimu kwa pande zote kama vile serikalini,wazazi na
wadau wa elimu.
Kwa
upande wake Afisa Elimu wa shule za msingi Mary Mathew alisema kuwa
pamoja na shule hizo kufanya vibaya serikali itaendelea kutatua
changamoto zilizopo ili wilaya hiyo iweze kufanya vizuri katika sekta ya
elimu.
No comments:
Post a Comment