TANGAZO


Tuesday, May 13, 2014

Rais wa Zanzibar, Dk. Shein afunga Mafunzo Maalum ya Maofisa wa KMKM, Kambi ya Kama mjini Unguja


* Asema nia kuimarisha maslahi ya watumishi wa Idara za SMZ

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akimvalisha Cheo cha Luteni Usu,  Abdallah Mohammed Mussa wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), katika sherehe za ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa 97 (Special Duty), mkupuo wa saba (7) katika kambi ya KMKM Kama, Wilaya ya Magharibi mjini Unguja leo. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu Zanzibar)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akimvalisha Cheo cha Luteni usu  Said Mohammed Omar wa JKU katika sherehe za ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa 97 (Special Duty), mkupuo wa saba (7) katika kambi ya KMKM Kama  Wilaya ya Magharibi Unguja leo.
Miongoni mwa Maafisa wanafunzi  97 waliohitimu mafunzo  ya kijeshi wakitoa salamu ya heshma kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) mara alipowasili katika uwanja wa Mafunzo kambi ya Kama Wilaya ya magharibi Unguja leo kuwafungia mafunzo yao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakisimama wakati gwaride la Maafisa wanafunzi wakipita mbele kwa heshima katika hafla ya  ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa (Special Duty) mkupuo wa saba(7) leo yaliyojumuisha wahitimu 97, katika uwanja wa mafunzo kambi ya  KMKM  Kama Wilaya ya Magharibi Unguja.
Kikisi cha Bendera cha  Maafisa wanafunzi wakipita mbele kwa heshima katika hafla ya  ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa (Special Duty) mkupuo wa saba(7) leo yaliyojumuisha wahitimu 97, wakipita mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwa mgeni rasmi katika uwanja wa mafunzo kambi ya  KMKM   Kama Wilaya ya Magharibi Unguja.
Maafisa wanafunzi wakitoa  heshima ya gwaride maalum katika hafla ya ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa (Special Duty) mkupuo wa saba(7) leo yaliyojumuisha wahitimu 97,wakipita mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwa mgeni rasmi katika uwanja wa mafunzo kambi ya  KMKM   Kama Wilaya ya Magharibi Unguja.
Maafisa wanafunzi wakitoa  heshima ya gwaride maalum katika hafla ya ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa (Special Duty) mkupuo wa saba(7) leo yaliyojumuisha wahitimu 97, wakipita mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwa mgeni rasmi katika uwanja wa mafunzo kambi ya  KMKM   Kama Wilaya ya Magharibi Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Kassim Juma Khamis,akiwa ni miongoni mwa Maafisa waliofanya vizuri zaidi katika mafunzo,wakati wa  ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa (Special Duty) mkupuo wa saba(7) leo, viwanja wa mafunzo kambi ya KMKM Kama Wilaya ya Magharibi  Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Hassan Omar Othman,akiwa ni miongoni mwa Maafisa waliofanya vizuri zaidi katika mafunzo, wakati wa  ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa (Special Duty), mkupuo wa saba(7) leo, viwanja wa mafunzo kambi ya KMKM Kama Wilaya ya Magharibi  Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati wa  ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa (Special Duty), mkupuo wa saba(7) leo, viwanja wa mafunzi kambi ya KMKM Kama Wilaya ya Magharibi  Unguja,(kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum  za SMZ, Haji Omar Kheri na Mkuu wa KMKM Komodore Hassan Mussa(kulia).
Baadhi ya wananchi walioalikwa katika hafla ya sherehe za ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa (Special Duty) mkupuo wa saba (7) katika kambi ya KMKM Kama Wilaya ya Magharibi Unguja leo.
Baadhi ya Viongozi na wananchi walioalikwa katika hafla ya sherehe za ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa 97, (Special Duty), mkupuo wa saba (7) katika kambi ya KMKM Kama  Wilaya ya Magharibi Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu KMKM alipowasili katika kambi ya KMKM Kama katika ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa (Special Duty) mkupuo wa saba(7) leo,(katikti) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheri.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akipokea salamu ya hesha ya gwaride la Maafisa wakati ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa (Special Duty) mkupuo wa saba (7) katika kambi ya KMKM Kama  Wilaya ya Magharibi Unguja leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la Maalum wakati wa ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa (Special Duty) mkupuo wa saba (7) katika kambi ya KMKM Kama  Wilaya ya Magharibi Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein alipokuwa akiwatunuku  Kamisheni Maafisa Wanafunzi waliohitimu mafunzo ya awali katika kambi ya KmKm kama leo, alipoyafunga mafunzo hayo katika mkupuo wa saba (7) wilaya ya Magharibi Unguja.
Makamanda wa KmKm waliohudhuria katika sherehe za ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa (Special Duty) mkupuo wa saba (7) katika kambi ya KMKM Kama Wilaya ya Magharibi Unguja leo.

Na Said Ameir, Zanzibar
Serikali imesema itaendelea kuchukua hatua kila inapowezekana ili kuimarisha mazingira ya kazi pamoja na maslahi ya watumishi wa vikosi vya Idara maalum vya SMZ lengo likiwa ni kuviwezesha vikosi hivyo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kwa weledi zaidi.
Akizungumza katika hafla ya ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maofisa wa Idara hizo na kutoa Kamisheni kwa wahitimu leo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alisema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha mazingira ya Idara hizo yanalingana na mazingira ya sasa ya utendaji kazi ambayo yanayozingatia maendeleo ya sayansi na tekinolojia.
“Serikali itafanya kila jitihada ili wapiganaji wetu tuweze kuwaandalia mafunzo ya fani mbalimbali hasa yanayoendana na sayansi na tekinolojia kwa kuwa azma yake ni kuwa na Idara za SMZ zenye nyenzo na vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi ili kuziwezesha kutekeleza majukumu yake ipasavyo”Dk. Shein alieleza.
Alieleza kuridhishwa kwake na kazi nzuri inayofanywa Idara hizo katika kutekeleza majukumu yake yakiwemo ya kusimamia amani na utulivu, ulinzi wa uchumi, kusaidia kutoa huduma za jamii kama vile afya na elimu pamoja na huduma wakati wa maafa.
Dk. Shein aliwapongeza askari wa Idara hizo Maalum kwa kukabiliana vyema na magendo ya karafuu ambapo alieleza matokeo ya jitihda zao ni  kuongezeka kwa pato la Serikali.
Hata hivyo alizitaka Idara hizo kuongeza kasi ya ulinzi hasa kukabiliana na vitendo vya baadhi ya wafanyabiashara wanaokwepa kodi kwa kuingiza na kupitisha bidhaa kinyume na sheria.
“Lazima tuongeze jitihada katika kukabiliana na vitendo hivi ambavyo vinalikosesha taifa kiasi kikubwa cha mapato kutokana na uingizaji na upitishaji wa bidhaa kupitia bandari zisizo rasmi” Dk. Shein alisisitiza.
Kwa upande mwingine alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa vikosi vya ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na Idara Maalum za SMZ ili kukomesha hujuma hizo na uhalifu mwingine na kuwakumbusha kuwa suala la ulinzi wa nchi ni jukumu la kila mwananchi.
Katika hafla hiyo iliyofanyika huko katika kambi ya KMKM iliyopo Kama Wilaya ya Maghribi Unguja, Dk. Shein aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kuthibitisha kwa vitendo kile walichojifunza kwa kutekeleza wajibu wao kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.
Kwa upande wake Mkuu KMKM Comodor Hassan Mzee alieleza kuwa askari waliopewa kamisheni wamejengewa uwezo mkubwa kupitia mafunzo hayo ambapo sasa wana uwezo wa kuongoza vyema askari walio chini yao.
Akitoa maelezo kuhusu mafunzo hayo Mkuu wa Mafunzo Mohamed Ali Bakari alieleza kuwa wahitimu wote wamemaliza vyema mafunzo yao kwa kufaulu mafunzo ya vitendo na nadharia darasani.
Alieleza kuwa jumla ya wahitimu 97 kati ya washiriki 100 wamemaliza mafunzo hayo ambao ni kutoka Idara tatu za SMZ ambazo ni Jeshi la Kujenga Uchumi-JKU, Kikosi cha Valantia-KVZ na KMKM.
Katika hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa pia na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, Dk. Shein alitoa kamisheni kwa wahitimu, zawadi kwa wahitimu waliofanya vyema, alikagua gwaride, na pia kuangalia  maonesho kutoka askari wa Idara hizo.  

No comments:

Post a Comment